Sunday, December 1, 2013

Wana CCM Vyuo Vikuu Morogoro wateta na Waziri Dk. Nchimbi

PIX 1
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Morogoro. Waziri Nchimbi aliwasikiliza maoni yao pamoja na maswali ambayo yalilenga kuimarisha chama chao mkoani humo. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Mount Uluguru mjini Morogoro. Picha na Felix Mwagara.
PIX 2
PIX 3
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) ambaye ni mwana CCM wa Umoja wa Vijana wa Vyuo Vikuu mkoani Morogoro akimuuliza maswali ya kuimarisha chama Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wapili kushoto-meza kuu). Waziri Nchimbi aliwasikiliza maoni na maswali mbalimbali wanafunzi hao ambayo yalilenga kuimarisha chama hicho mkoani humo. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Mount Uluguru mjini Morogoro. Picha na Felix Mwagara.
PIX 4
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (Watatu kulia-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Morogoro. Waziri Nchimbi aliyasikiliza maoni pamoja na maswali yao ambayo yalilenga kuimarisha chama chao mkoani humo. Kikao cha kuimarisha chama chao kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Mount Uluguru mjini Morogoro. Picha zote na Felix Mwagara.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About