Tuesday, January 21, 2014

AJALI MBAYA YA BASI LA ABIRIA MKOANI LINDI
Jumla ya watu 9 wameripotiwa kufariki  na wengine zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la abiria kupinduka mkoani Lindi kutokana na kutaka kulikwepa lori walilokuwa wakipishana nalo eneo la ajali.
Basi hilo la kampuni ya Alhamdulilah linalofanya safari zake kati ya Mtwara Dar es salaam.

Ajali hiyo ilitoekea eneo la Mambulu mkoani Lindi majira ya mchana leo.
Imedaiwa chanzo cha ajali ni basi hilo kupishana na lori na kupoteza mwelekeo na hatima yake kupinduka kutokana na utelezi uliokuwepo uliotokana na mvua iliyokuwa ikinyesha mkoani humo.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About