Welcome to our online store Portal

Template Information

Saturday, January 4, 2014

CHADEMA YAPIGWA STOP NA MAHAKAMA KUU YA TZ, YAFUKUZA KIONGOZI MWINGINE

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe akiwa na Mwanasheria wake,Albert Msando(katikati)na Mwanasheria wa Chadema,Peter Kibatara(kushoto) wakiwa nje chumba cha Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam jana wakisubiri maamuzi ya Jaji kuhusu madai ya Zitto ya Kupinga Kamati Kuu ya Chama hicho kumjadili.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji John Utamwa baada ya kupokea maombi ya Zitto kupitia kwa Wakili wake, Albert Msando kutaka rufaa yake aliyoiwasilisha Baraza Kuu kusikilizwa kwanza kabla ya kufanyika uamuzi mwingineMahakama Kuu Tanzania, imeizuia kwa muda Kamati Kuu ya Chadema kujadili ajenda zozote zinazomhusu aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe hadi ombi lake la rufaa litakaposikilizwa. 
Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji John Utamwa baada ya kupokea maombi ya Zitto kupitia kwa Wakili wake, Albert Msando kutaka rufaa yake aliyoiwasilisha Baraza Kuu kusikilizwa kwanza kabla ya kufanyika uamuzi mwingine.
Kamati Kuu ya chama hicho, ilipanga kukutana leo ikiwa na ajenda kuu tatu; kupanga mpangokazi wa chama kwa mwaka 2014, kupokea utetezi wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa
Zuio hilo lilikuja pia baada ya kutupiliwa mbali maombi ya pingamizi la Chadema lililowasilishwa na Mkurugenzi wa Katiba na Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Peter Kibatala.
Akizungumza jana baada ya uamuzi huo wa Mahakama, Mwanasheria Mkuu Chadema, Tundu Lissu alisema hakuna jinsi zaidi ya kukubaliana na uamuzi huo... “Tumekubali kutokumjadili Zitto lakini tuliomba Mahakama iruhusu kuhojiwa kwa Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.
Zitto alifungua kesi Mahakama Kuu akiiomba iizuie Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Katibu Mkuu pamoja na Kamati Kuu ya Chadema kumjadili, kumchukulia hatua yoyote kuhusu uanachama wake hadi hapo rufaa yake aliyoikata Baraza Kuu la Chadema itakaposikilizwa.
Pia katika maombi yake, Zitto alitaka Mahakama kuzuia kwa njia yoyote, Kamati Kuu kumwingilia katika utekelezaji wa majukumu yake ya Ubunge wa Kigoma Kaskazini.
Mbali na ombi hilo, pia aliiomba Mahakama kumwamuru Katibu Mkuu wa Chadema ampatie nakala ya mashtaka na maelezo ya uamuzi uliofikiwa na Kamati Kuu Novemba 22, 2013 wa kumwondolea nyadhifa zake ili aweze kuwasilisha rufaa yake Baraza Kuu la Chadema kupinga uamuzi huo.
Zitto kupitia wakili wake, Msando alifungua kesi hiyo ya madai namba moja ya mwaka 2014 akipinga uamuzi huo wa Novemba 22, 2013 pamoja na hatua zaidi zilizoagizwa kuchukuliwa dhidi yake kuhusiana na uanachama katika chama chake. Walalamikiwa ni Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chadema.
Walalamikiwa hao, kupitia kwa Lissu na Kibatala waliwasilisha pingamizi wakiiomba Mahakama itupilie mbali kesi hiyo kwa madai kuwa vifungu vilivyotumiwa katika kuwasilisha maombi hayo havikuwa sahihi.
Pia waliomba Mahakama hiyo kutupilia mbali kesi hiyo kwa madai kuwa hati ya kiapo iliyotumiwa kuwasilisha maombi hayo ina upungufu wa kisheria na kwamba Mahakama hiyo haina uwezo wa kuyasikiliza.
Zitto kupitia Wakili Msando, alisisitiza kuiomba Mahakama hiyo kuamuru Kamati Kuu ya Chadema na uongozi wowote wa chama hicho kutokuingilia, kujadili au kuchunguza suala lolote la uanachama wake hadi hapo rufaa yake itakapopitiwa na Baraza Kuu la Chadema.
Alisema bado ni Mbunge halali wa Kigoma Kaskazini na aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama hicho hadi Novemba 22, 2013, Kamati Kuu ya Chadema ilipoamuru avuliwe nyadhifa zote alizokuwa nazo na kuagiza hatua zaidi zichukuliwe kuhusiana na uanachama wake. Uamuzi huo uliwasilishwa kwake kwa maandishi kupitia kwa Mkurugenzi wa Habari wa Chadema, John Mnyika na Lissu alipozungumza na vyombo vya habari Novemba 26, 2013 alitangaza madai yao kisha kutoa siku 14 kwa watuhumiwa kujibu hoja zao.

Akizungumza jana, Dk Kitila Mkumbo alisema amejiandaa kisaikolojia na ana subiri kwenda kwenye kikao hicho kusikiliza na kujibu maswali yoyote atakayoulizwa kwa kuwa huo siyo mtihani ambao anatakiwa kujiandaa kabla ya kwenda kuufanya.
Alipoulizwa kama amejiandaa kupokea uamuzi wowote utakaotolewa, Mkumbo alisema: “Suala kwamba haki itatendeka au la, nitalizungumza nikitoka kwenye kikao.”
Kwa upande wake, Samson Mwigamba alisema ana uhakika kuwa haki haitatendeka kwa sababu haikutendeka tangu mwanzo alipowasilisha malalamiko yake kwenye kamati hiyo.
“Haki haiwezi kutendeka, wakati ule nilikata rufaa, badala ya kuijadili, walinivua uongozi,” alisema Mwigamba.

Baraza la Uongozi la Chadema Wilaya ya Tanga, limemvua wadhifa Katibu wa Wilaya hiyo, Khalid Rashid kwa makosa 10 likiwamo la kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kumvua madaraka Zitto. Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tanga, Said Mbweto, alisema Khalid amekosa sifa za kuwa Katibu wa Wilaya.
Aliyataja baadhi ya makosa yake kuwa ni kulivunjia heshima Baraza la Wazee wa Mkoa, kwenda Pangani kufanya mkutano kinyume na sheria, kupinga kufukuzwa kwa Zitto, kuandika barua ya dharau kwa uongozi wa Chadema Mkoa na kukusanya saini za wanachama kwa kisingizio kuwa ni agizo la Chadema Taifa.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop