Saturday, January 4, 2014

MABOMU YAENDELEA KUWATESA WAKAZI WA DAR

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Bomu la kurushwa kwa mkono lililokuwa katika njia ya watembea kwa miguu katika makutano ya barabara ya Shekilango na Morogoro jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Herman 

Wakazi na wapita njia katika makutano ya barabara ya Morogoro na Shekilango,  jana walikumbwa na hofu kufuatia kuzagaa kwa taarifa ya kuonekana kwa kitu kinachodhaniwa kuwa  ni bomu la kutupa kwa mkono ambalo lilikuwa ardhini eneo hilo, jirani na maghorofa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Heka heka hiyo ilizuka kunako saa tano na robo za asubuhi na kudumu kwa zaidi ya saa moja, kulitokana na mkazi mmoja wa jijini, Alfani Zidadu kuona kitu kilichokuwa ardhini ambacho kilishabihiana na bomu hali ambayo ilimfanya awasiliane na mama yake ambaye alikuwa na miadi ya kukutana nae eneo hilo.
Zidadu alisema kuwa mama yake, Asha Zidadu alikuwa anakaribia eneo la tukio na alipofika eneo hilo alimuonyesha kitu hicho na muda mfupi baadae aliwasiliana na polisi Urafiki ambao walifika na baada ya kukiona kitu hicho walizungushia uzio eneo hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alikiri kuwepo kwa tukio hilo lakini alikataa kuingia kwa undani kuhusiana na kitu hicho iwapo ni bomu au la kwa madai kuwa polisi wanakifanyia uchunguzi ili kujua ni kitu gani hasa.
“Kwa sasa siwezi kusema kuwa ni bomu au la isipokuwa tunasubiri uchunguzi kujua kilikuwa ni kitu gani hasa” alisema Kamanda Wambura na kubainisha kuwa kwa sasa anaweza kusema kuwa ni mabaki ya vipande vya mabati.
Mwananchi baada ya kufika katika eneo hilo lilishuhudia askari wakiimarisha ulinzi katia eno hilo huku wananchi wakitawanywa na kutakiwa kuwepo mita 100 kutoka eneo la tukio kwa maelezo kuwa iwapo litalipuka linaweza kusababisha wakapoteza maisha.
“Ondokeni hapa, simameni huko” alisema askari aliyekuwa ameshika bunduki ya kufyatulia mabomu ya machozi na kuongeza kuwa wateguaji wangefika eneo hilo wakati wowote na iwapo makosa yatafanyika wakati wa kulitegua wananchi walio jirani na eneo hilo wangeweza kupoteza maisha.
Askari wa kikosi maalum cha kutegua mabomu ilifika eneo hilo na kuanza kazi ya kuchimba na kuweka tahadhari zote za kuzuia lisilipuke na msimamizi wa operesheni hiyo ambaye al     ikataa kutaja jina lake aliwataka askari wanaotegua kuhakikisha pini ya bomu hilo imekaza na ipo katika sehemu yake.
“Hakikisheni pini imekaza na hata kama imelegea irudishieni” alisema msimamizi huyo na baada ya kufukuliwa kwa kitu hicho kinachodhaniwa kuwa ni bomu, kiliwekwa katika mfuko wa karatasi na kufungiwa katika sanduku maalum ambalo walifika nalo eneo hilo la tukio.
Baadhi ya watu waliozungumza na Mwananchi walionyeha mshangao kuhusiana na kitu hicho na kuhoji kuwa iwapo ni bomu ambalo limetegwa lilikuwa limemlenga nani kwani wengi wa watu wanaoshinda eneo hilo ni wale wa bodaboda na abiria wanaosubiria mabasi ya kwenda Mwenge kupitia Sinza.
“Sijui mlengwa alikuwa nani lakini ni bomu kabisa kama yale ambayo huwa tunayaona katika luninga” alisema muosha magari katika eneo hio aliyejitambulisha kwa jina la Ibrahim Momba na kuongeza kuwa huenda kuna harufu ya ugaidi katrika tukio hilo.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About