Ujenzi wa Daraja la Kigamboni unatarajia kukamilika Julai mwakani badala ya Januari mwakani.
Awali ilielezwa kuwa kazi hiyo ingekamilika
Januari mwakani lakini changamoto walizokutana nazo wahandisi chini ya
bahari zimesababisha ujenzi kuchelewa kukamilika.
Hayo yalibainika juzi wakati katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi, Mhandisi Mussa Iyombe, alipotembele ujenzi wa Daraja la
Kigamboni lenye urefu wa wa mita 600 ili kujionea maendeleo
yaliyofikiwa.
Katika eneo hilo, Mhandisi Iyombe aliwakemea
wananchi watatu walikuwa wakipinga kuondoka katika eneo hilo ili kupisha
mradi huo kwa madai kuwa hawakufanyiwa tathmini ya uhakika kuhusu mali
zao.
Akizungumzia tatizo hilo, alisema kwa sasa watu
hao wameshafanyiwa tathimini na kwamba kilichobaki ni ripoti ya Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,kukabidhiwa kwa kwa watu hao ili
hatimaye, waweze kuondoka kwa hiyari.
Mhandisi Iyombe aliwaonya watu hao wasijaribu tena
kutaka kuchelewesha mradi huo na kwamba vinginevyo Serikali itatumia
nguvu kuwaondoa.
Alisema mbali na changamoto hizo, bado wakandarasi
wamekuwa wakiendelea vizuri na kwamba kazi iliyofanyika inatoa
matumaini kwa Watanzania.
0 comments:
Post a Comment