Saturday, January 11, 2014

DR. BILALI AFUNGUA SHULE YA SEKONDAR KIEMBE SAMAKI ZNZ


05
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar jana Jan 10, 2014. Kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamhuna. (Picha na OMR).
06
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la Msingi la shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar.
01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipokuwa akitembelea chumba cha Maabara baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar.
02
03
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki, Amina Salum Khalfan, wakati alipotembelea katika chumba cha Mawasiliano na mafunzo ya Kompyuta cha shule hiyo, baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika jana.
2
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya vitabu vya kumbukumbu za Maktaba ya Shule mpya ya Sekondari ya Kiembe Samaki wakati alipotembelea chumba hicho cha Maktaba baada ya kuzindua rasmi Shule hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo mjini Zanzibar jana Jan 10, 2014. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Amina Salum Khalfan.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea chumba cha Maabala kati ya vyumba vinne vilivyopo shuleni hapo.
8
Wanafunzi wa shule ya Msingi Kiembe Samaki, wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kiembe Samaki,  baada ya uzinduzi rasmi wa shule hiyo uliofanyika jana Jan 10, 2014, mjini Zanzibar. (Picha na OMR).
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About