Rais Jakaya Kikwete amekutana na mabalozi 49 kutoka katika mbalimbali duniani, ambapo alitumia fursa hiyo kuzungumza nao kuhusu maendeleo ya nchi.
Rais Kikwete alikutana na mabalozi hao katika
hafla mwaka mpya iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam na
katika mazungumzo yake alisisitiza kudumisha ushirikiano wa kimaendeleo
baina ya nchi hizo.
Alitumia fursa hiyo kuwaeleza mabalozi hao mambo
mbalimbali yaliyofanyika nchini mwaka 2013, akigusia mkakato wa Katiba
Mpya, ambapo alisema hadi Mei mwaka huu, Bunge la Katiba litakuwa
limemalizika.
Alisema kumalizima kwa Bunge hilo, kutatoa fursa ya kuanza kwa shughuli ya ukusanyaji wa maoni.
Alizungumzia pia jisni Tanzania ilivyopiga hatua
katika sekta ya elimu, kujenga barabara, kutoa huduma za maji na umeme
na kupambana na ujagili na kudhibiti rushwa.
“Hata ugonjwa wa malaria umepungua kutoka asilimia
18 hadi asilimia 8, hata maambukizi ya Ukimwi yamekuwa chini kwa
asilimia 5, lakini hatuwezi kujivunia katika hilo, tutapambana,”
alisema.
Alisema vifo vya watoto pia vimepungua kwa kiwango
kikubwa kutoka watoto 165 kati ya 1,000 mwaka 1990 hadi watoto 54 kati
ya 1,000 mwaka 2013, na kwamba Serikali inafanya uchunguzi wa magonjwa
mbalimbali ili kuokoa maisha ya wananchi wake.
Pia aligusia ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara
hadi Dar es Salaam na kusema kuwa mpaka sasa asilimia 24 wanatumia
nishati ya umeme.
“Mpaka kufikia mwaka 2015 tunataka kufikisha
asilimia 30 ya watu wanaotumia umeme,” alisema. Alisema sekta
zinazoguswa na mpango wa Matokeo Makubwa Sasa(BRN) zitakuwa kwa kiwango
kikubwa kwa muda wa miaka mitano.
0 comments:
Post a Comment