Saturday, January 11, 2014

57 WAKAMATWA KILIMANJARO KUINGIA NCHINI KINYUME NA SHERIA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro inawashikilia wahamiaji haramu 57 raia wa Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.
Ofisa Uhamiaji, Johaness Msumule amekiri kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu na kusema, walikamatwa Januari 10 mwaka huu saa saba usiku katika Kijiji cha Ghona Chekereni, wilayani Moshi mkoani hapa. PICHA NA MAKTABA
Msumule alisema kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu kumetokana na taarifa ya watu wema, akiwamo Mwenyekiti wa Kijiji cha Ghona, Ramadhan Abdallah aliyewataarifu kuwapo kwa watu hao kandokando ya Barabara ya Moshi/Dar es Salaam wakisubiri usafiri.
“Tulipigiwa simu usiku wa manane na kuelezwa uwepo wa wahamiaji haramu, na sisi tulichukua magari tukishirikiana na Jeshi la Polisi na tulipofika tuliwakuta wakiwa chini ya ulinzi wa sungusungu wa kijiji,” alisema Msumule.
Alisema wahamiaji hao haramu husafirishwa kwa pikipiki kwa njia za panya na kufikishwa eneo la chekereni, ambalo ni moja ya vituo vyao vikuu na baadaye kupakiwa kwenye malori kwa lengo la kusafiri kwenda Dar es Salaam na baadaye kuelekea Afrika Kusini.
“Mara baada ya kuwakamata lilitokea Fuso kwa lengo la kuwachukua, lakini walipowaona sungusungu gari hilo lilikimbia sambamba na mtu aliyesadikiwa kuwa kinara wa kuwasafirisha wahamiaji,” alisema
Alisema kutokana na maeneo ya Chekereni, Kifaru na Makuyuni kuwa kitovu cha kuwahifadhi wahamiaji haramu,Ofisi ya Uhamiaji imelenga kuweka doria ya usiku kwa kutumia askari na magari kuanzia Januari 13 mwaka huu lengo likiwa ni kukamata vinara wanaowasafirisha na kumaliza tatizo hilo.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About