Saturday, January 11, 2014

MADIWANI MWANZA WAIGOMEA BAJETI

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wameshindwa kupitisha Makadirio ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2014/2015 iliyokadiriwa kukusanya Sh87 bilioni kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato vya halmashauri pamoja na ruzuku kutoka serikalini.
Baraza hilo lilitarajiwa kupitisha rasimu hiyo ya bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 zikiwa pamoja na ruzuku kutoka Serikali Kuu na wahisani Sh77.2 bilioni matumizi ya halmashauri Sh9.1 bilioni pamoja na michango ya wananchi Sh239.3.
Akisoma bajeti hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Karsan Hida alisema kuwa fedha hizo zinatarajiwa kukusanywa kutoka katika vyanzo vya mapato vya halmashauri pamoja na ada mbalimbali.
Alisema kuwa kipaumbele walichoweka ni pamoja na ujenzi wa Jengo la Wodi ya Wanaume katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana itakayogharimu Sh2 bilioni, ujenzi wa jengo la Mahakama ya Jaji Sh2 bilioni.
Hida pia alisema kuwa halmashauri imelenga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na utoaji wa huduma kama Afya, Elimu, Kilimo na Mifugo, ushirika pamoja na maendeleo ya jamii na sekta ya uvuvi katika halmashauri hiyo.
Wakichangia katika bajeti hiyo, Diwani wa Igoma Adamu Chagulani alisema kuwa bajeti hiyo haijitoshelezi, kwani vyanzo vingi vya mapato vimeachwa bila kutolewa ufafanuzi katika makabrasha hali inayowapa wasiwasi madiwani kuijadili rasimu hiyo.
Walipendekeza bajeti hiyo kuandaliwa upya ili ikidhi mahitaji ya wananchi wa Mwanza, huku wakiwataka kuangalia upya miradi ambayo haijakamilika kuweza kuitengea bajeti.
“Kuna nyumba chache tu zinalipa kodi, wakati zingine zaidi ya 800 hazilipi kodi kama inavyotakiwa,” walisema madiwani hao.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Mwanza, Maria Hewa alisema kuwa kuna vyanzo vingi vya mapato kama shule za binafsi hazitozwi kodi bila kutaja sababu husika.
“Mkurugenzi ufanye kazi na watumishi wako ili tufike mahali tunapata mafanikio. Tumeungana vyama vyote, tunataka bajeti irudi na ichambuliwe kwa upya na kuangalia vyanzo vyote vya mapato,” alisema Hewa.
Akiahirisha kikao hicho, Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula alisema kuwa kilichofanyika ni kurekebisha matatizo ambayo yataisaidia halmashauri ili kuweza kupata mafanikio.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About