Welcome to our online store Portal

Template Information

Monday, January 6, 2014

MCHINA KIZIMBANI KWA KUCHANA NOTI YA ELFU KUMI

http://azizicompdoc.blogspot.com/http://azizicompdoc.blogspot.com/
Raia wa China ambaye ni meneja uzalishaji katika kampuni ya ujenzi  Shen Hai,46, amepandishwa kizimbani kwa kosa la kuchana noti ya shilingi 10,000 ambayo ni mali ya Serikali ya Tanzania.
Akisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mkoa Janeth Masesa, Mwendesha Mashtaka wa Serikali,   Castus Ndamugobas alidai kuwa Mchina huyo alitenda kosa hilo mnamo Desemba 3 mwaka jana katika maeneo ya uwanja wa ndege Wilaya ya Ilemela majira ya saa 10:30 jioni ambapo kwa makusudi aliichana noti hiyo  yenye namba AY3748043, ambayo  thamani yake ni Sh10,000 mali ya Serikali ya Tanzania.
Mshtakiwa huyo ambaye ni meneja mzalishaji aliyeajiriwa na Serikali ya Tanzania ili kufanya ukarabati katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza, alikana mashtaka yote na alirudishwa rumande baada ya kutokidhi masharti ya dhamana na hakimu Masesa aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 8 mwaka huu ambapo itafikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa tena.
Kitendo  hicho cha raia huyo wa China kuchana noti kilionyesha dharau kwa nchi ya Tanzania na raia wake.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop