Wednesday, January 15, 2014

MDEE TIBAIJUKA WAVAANA KUHUSU ARDHI

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee amemshukia Waziri wa wizara hiyo, Profesa Anna Tibaijuka kwa kushindwa kutatua mgogoro wa shamba la Kapunga mkoani Mbeya na badala yake ameukuza.

Kwa mujibu taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyotoa jana, Mdee alisisitiza kuwa ripoti zilizotolewa kwenye vyombo vya habari wiki iliyopita zinathibitisha kukua kwa mgogoro huo hasa baada ya wananchi kunung’unika mbele ya waziri huyo wakati wa ziara yake. Mdee alisema kuwa hatua hiyo imeonyesha kuwa mgogoro huo wa Shamba la Kapunga lililopo wilayani Mbarali, mkoani Mbeya umechukua sura mpya kwa sasa kwa kuigharimu taswira ya kisiasa ya Waziri Profesa Tibaijuka ambaye wananchi walimlaumu kutokana na kubadili msimamo juu ya suala hilo.
“Taarifa zimeonyesha kwamba mgogoro huo bado unatokota, tena safari hii ukionekana dhahiri kuigharimu Serikali ya CCM kwa kuonyesha kuwa sera zake za kusimamia ardhi zimeshindwa na haiwezi kuwajibika kwa ajili ya wananchi,” alisema Mdee, ambaye pia ni Mbunge wa Kawe kupitia Chadema.
Mdee alisema iliripotiwa kuwa Profesa Tibaijuka hakuwafurahisha wananchi wa Kapunga baada ya kuingia ndani ya gari la mwekezaji ambaye ndiye yuko kwenye mgogoro na wananchi kugombania eneo hilo, kisha aliposhuka akawa amebadili msimamo aliokuwa nao awali .
Alisema Waziri Tibaijuka alitakiwa kwenda Kapunga huku akiujua ukweli wa chimbuko la mgogoro huo ni serikali yenyewe kupitia Nafco ambayo iliuza ardhi kwa mwekezaji (hekta 7,370) na kusajili na kupata hati kwa eneo lote ikiwamo hekta 1870 za kijiji.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About