Wednesday, January 22, 2014

TIGO YATOA ZAIDI YA NUSU BILIONI KWA WATEJA WAKE WALIOSHINDA


1
Mshindi wa shilingi milioni 10 katika promosheni ya Tigo ‘Shinda Kitita na Tigo Pesa’ Bi. Margaret Mbungu Mwanjala akifurahia zawadi ya kitita cha fedha alizokabidhiwa na Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa Bi. Mary Rutta (kulia) mapema leo jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa wateja 1,590 wameweza kujishindia zawadi ya fedha taslimu milioni 560 huku milioni 560 zingine zikibakia kushindaniwa katika wiki tatu zijazo.
2
Mshindi wa shilingi milioni mbili katika promosheni ya Tigo ‘Shinda Kitita na Tigo Pesa’ Bw. Emmanuel William Mabojola (kushoto) akihesabu pesa alizojishindia kwenye shindano hilo mapema leo jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa Bi. Mary Rutta. 
3
Bi. Vaileth Methusela Mkuku naye akihesabu shilingi milioni mbili alizoshinda kutoka Tigo. Zawadi zinazoshindaniwa ni za shilingi 200,000/- kwa wateja 50 kila siku, milioni 2 kwa wateja 20 kila wiki na zawadi ya juu kabisa ni ya fedha taslimu milioni 10 wanayoshinda wateja watano kila baada ya wiki mbili. 
4
Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa Bi. Mary Rutta (kulia) akimpongeza mshindi wa shilingi milioni mbili katika promosheni ya ‘Shinda Kitita na Tigo Pesa’ Bw. Boniface Bembele Mwita aliyekabidhiwa kitita chake mapema leo jijini Dar es Salaam. Kushiriki katika promosheni hii mteja wa Tigo anatakiwa kutumia akaunti yake ya Tigo Pesa kutuma fedha, kununua bidhaa, kuongeza salio na kulipia bili za huduma mbali mbali.
Ikiwa ni mwezi tu tangu promosheni ya Tigo ‘Cheza Kwa Furaha Unaposhinda Kitita na Tigo Pesa’ ilipozinduliwa, wateja 1,590 wameweza kujishindia zawadi ya fedha taslimu milioni 560 huku milioni 560 zingine zikibakia kushindaniwa katika wiki tatu zijazo.  

Akizungumzia muenendo wa promosheni hiyo katika makao makuu ya kampuni hiyo ya simu leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Promosheni wa Tigo Pesa Mary Rutta amesema kwamba zawadi zilizoshindaniwa ni za shilingi 200,000/- kwa wateja 50 kila siku, milioni 2 kwa wateja 20 kila wiki na zawadi ya juu kabisa ni ya fedha taslimu milioni 10 wanayoshinda wateja watano kila baada ya wiki mbili.
“Tunazidi kushuhudia wateja wengi zaidi wakifurahia kushinda hizi zawadi za fedha taslimu kwa kufanya miamala kupitia akaunti zao za Tigo Pesa. Hii ni pamoja na kutuma fedha, kununua bidhaa, kuongeza salio au kulipia bili mbali mbali. Tunafuraha kwamba washindi wametoka mikoa yote nchini na kumekuwa na uwiano mzuri baina ya washindi kutoka mijini na vijijini,” alisema Rutta.

Mratibu huyo wa promosheni aliendelea kutoa wito kwa wateja wa Tigo kuendelea kufanya miamala ya Tigo Pesa akisisitiza kwamba zimesalia wiki tatu tu promosheni hii kuisha katikati ya mwezi Februari.
“Promosheni yetu inadhihirisha kwamba Tigo ni kampuni ambayo inaendelea kuweka jitihada ya kila siku katika kukidhi matarajio ya wateja wake. Tunaamini kuwa promosheni hii kwa namna moja au nyingine imeweza kubadilisha maisha ya washindi hawa 1,590 ambao wengi wao waliweza kupatiwa pesa zao wakati wa msimu wa Krismasi na Mwaka Mpya, muda ambao mahitaji ya kifedha huwa juu,” alisema.
Mkutano huu wa waandishi wa habari pia umehudhuriwa na washindi watano kati ya washindi 375 wa wiki iliyopita ambao walielezea promosheni hii kwamba ni “ya kweli”   na yenye “kufurahisha.” Washindi waliokuwepo wale walioshinda shilingi milioni mbili waliwemo Emmanuel William Mabojola, Boniface Bembele Mwita, Violeth Msela Mkuku and Amina Saida Aboud. Mwingine ni Margaret Mbungu Mwanjala aliyeshinda shilingi milioni 10.

“Ni kwa neema ya Mungu nimeweza kushinda hizi fedha. Hakika imekuja kwa kunistukiza, sikutarajia na sikuamini kabisa,” alisema Mwanjala aliyeshinda zawadi hiyo nono ya juu kabisa.
Ili kupata nafasi ya kushinda katika muda uliobaki wa promosheni hii, Rutta aliwasihi wateja wa Tigo “kuendelea kutumia akaunti zao za Tigo Pesa kwa ajili ya kutuma fedha, kununua bidhaa, kuongeza salio au kulipia bili mbali mbali, ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda.”
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About