Welcome to our online store Portal

Template Information

Wednesday, January 22, 2014

248 SINGIDA WAINGIA CCM


Sadifa Juma Khamis-
 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa -Sadifa Juma Khamis.
DSC05790
Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana CCM (UVCCM) wilaya ya Singida mjini,Ibrahimu Ramadhani akizumgumza kwenye mkutano wa wanachama wa CCM wa tawi la chuo cha uhasibu cha tawi la mkoa wa Singida.
DSC05778
Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana CCM (UVCCM) wilaya ya Singida,Ibrahimu Ramadhani (wa kwanza kushoto) akifurahia jambo na mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) CCM taifa kupitia UVCCM,Jonathan Nkya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa wanachama wa CCM chuo cha uhasibu tawi la mkoa wa Singida.
DSC05773
Baadhi ya wananchama wa CCM chuo cha uhasibu tawi la mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) CCM taifa, Jonathani Nkya (hayupo kwenye picha).

Mjumbe wa Halmashauri kuu (NEC) CCM taifa kupitia Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM), Jonathan Nkya amevuna wanachama wapya 248 waliojiunga na Chama Cha Mapinduzi.
Wanachama hao wapya, ni wanafunzi wa chuo cha Uhasibu tawi la mkoa wa Singida.
Akizungumza hivi karibuni na wanachama hao wapya wa CCM, Nkya aliwatahadharisha na wanasiasa ambao malengo yao ni kupandikiza sera ambazo zimekuwa chachu na chanzo cha migogoro katika vyuo mbalimbali.

Aliwataka wawe makini na wanasiasa hao wenye lengo la kujitafutia umaarufu binafsi kwa kupandikiza sera zisizokuwa na tija zaidi ya kupandikiza chuki na migogoro isiyoisha..
Katika hatua nyingine Mnec huyo, amewataka wanafunzi wa vyuo vya uhasibu watakaobahatika kuajiriwa na halmashauri za wilaya, manispaa na majiji, kutumia taaluma ya vizuri kudhibiti wizi wa fedha na umma, ambao unapigiwa kelele kila kona ya nchi.

Amesema fedha za umma zinazopelekwa kwenye halmashauri kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ni nyingi mno, lakini kiwango kikubwa cha fedha hizo, zinaishia kwenye mkono wa watumishi wasio waaminifu.
“Ninyi mkimaliza masomo yenu, muwe wazalendo wa kweli wa nchi yenu, katika kudhitibiti na kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yanayokusudiwa tu, na si vinginevyo” amesema Nkya ambaye ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Mzumbe.

Awali Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Singida mjini, Ibrahimu Ramadhani, aliwapongeza wanachama hao wapya kwa uamuzi wao wa busara wa kujiunga na chama chenye sera zinazotekelezeka.
Aidha amewahimiza kusoma kwa bidii na kwa malengo, kujiepusha kabisa na vitendo vitakavyochangia kufanya vibaya kwenye mitihani yao.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop