Mstahiki
Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh. Dk. Didas Masaburi (kulia) akikata
utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mashine maalum ya pili ya ‘TigoMatic’
inayopatikana Masaki jijini Dar es Salaam mapema. Kushoto ni Mkuu wa
Idara ya Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Zaem Khan.
Meneja
wa Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Henry Mboya akimuonyesha Mstahiki Meya wa
jiji la Dar es Salaam Mh. Dk. Didas Masaburi jinsi mashine ya TigoMatic
inavyoweza kufanya kazi katika kununua muda wa maongezi, kutuma na
kupokea pesa, kulipia bili za huduma mbali mbali na kupata laini mpya ya
simu.
Mstahiki
Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh. Dk. Didas Masaburi akionyesha kadi ya
kipaumbele ya Tigo ambayo inatolewa kwa wateja waliokaa na Tigo kwa
muda mrefu. Kadi hiyo inawezesha wateja kupatiwa huduma mbali mbali bila
kupanga foleni na kuondokana na usumbufu wa gharama ndogo ndogo pindi
watakapofika katika matawi yeyote ya Tigo kuhudumiwa.
stahiki
Meya wa jiji la Dar es Salaam Mh. Dk. Didas Masaburi akitoa hotuba
yake. Mstahiki Meya huyo aliipongeza Tigo kufanikiwa kuwa kampuni ya
simu ya kwanza nchini Tanzania kuanzisha huduma hiyo za mashine maalum
za TigoMatic.
Mkuu
wa Idara ya Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Zaem Khan akimshukuru Mstahiki
Meya, waandishi wa habari na wegeni wengine waalikwa kwa kufika katika
uzinduzi huo. Mashine ya TigoMatic itakuwa wazi kwa masaa ishirini na
nne kila siku.
Tigo
Tanzania imezindua mashine maalum ya pili ya TigoMatic inayowawezesha
wateja wake kulipia bili za huduma mbali mbali na kuongeza salio
itakayofanya kazi kwa masaa ishirini na nne kwa siku.
Uzinduzi
huo umehudhuriwa na Meya wa jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi,
ambaye ameipongeza Tigo kwa kuwa kampuni ya mawasiliano kwanza nchini
Tanzania kuanzisha huduma ya aina hiyo nchini.
“Ubunifu
huu wa Tigo si tu wa manufaa kwa wateja wake bali pia ni hatua mojawapo
kubwa ya kimaendeleo kwa nchi yetu katika matumizi ya teknolojia za
mawasiliano za kisasa duniani katika sekta ya mawasiliano,” alisema Dk
Masaburi.
Dk
Masaburi alisema huduma mbalimbali zitolewazo na makampuni ya simu
zikiwemo kupiga simu, SMS, intaneti pamoja na huduma za kutuma na
kupokea fedha zimeleta mageuzi chnaya katika ufanyaji biashara na
kuchangia kuboresha maisha ya mamilioni ya watanzania.
Akizungumza
katika uzinduzi huo uliofanyika katika tawi la huduma kwa wateja la
Tigo lililopo Masaki, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja Tigo Bw. Zaeem
Khan, amesema uzinduzi wa ‘TigoMatic’ utawawezesha wateja wa Masaki
kupata huduma za zitolewazo na Tigo kwa masaa ishirini na nne kwa siku.
“Habari
njema kwa watu wa Masaki ni kwamba hakutakuwa na ulazima tena kwa
wateja kukaa kwenye foleni kwa ajili ya kupata huduma kutoka kwenye
matawi yetu na sehemu nyinginezo za mauzo kwa sababu mashine hii ya
TigoMatic inatoa msaada wa mteja kujihudumia mwenyewe,” alisema Bw.
Khan.
Hii
ni mashine ya TigoMatic ya pili kuzinduliwa jijini Dar es Salaam na
kampuni ya simu Tigo. Mwezi uliopita Tigo ilikuwa kampuni ya simu ya
kwanza nchini kuzindua matumizi ya aina hii ya mashine ilipoanza kutoa
huduma hii katika tawi la makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko
Kijitonyama.
Akielezea
jinsi mashine hizo zinavyofanya kazi, Bw. Khan alisema TigoMatic ni
mashine ambazo mteja anaweza akajihudumia yeye mwenyewe kama ilivyo kwa
mashine za kibenki za ATM ambapo mteja anaweza akafanya miamala tofauti
tofauti bila kuhitaji kuhudumiwa na mfanyakazi wa benki. Alisema kwamba
wateja wa Tigo hawatakuwa na ulazima wa kujisajili upya kwa ajili ya
kutumia mashine hizo.
Khan
alisema kampuni inaazimia kuweka mashine zake katika matawi yake yote
ya huduma kwa wateja nchi nzima pamoja na sehemu za mikusanyiko mikubwa
ya watu kama vile maduka makubwa, stendi za mabasi, mitaani, viwanja vya
michezo na mahospitalini.
0 comments:
Post a Comment