Thursday, February 20, 2014

KAULI YA RAIS KIKWETE KUHUSU USHOGA


Akihojiwa  na CNN nchini Uingereza hivikaribuni wakati akihudhuria mkutano uliolenga kuongeza mapambano dhidi ya
ujangili, Rais Jakaya Kikwete amepigilia msumari wa moto akisema Tanzania haiko tayari kukubaliana na matakwa ya baadhi ya nchi za magharibi zinazotaka nchi za Afrika ziwe na sheria zinazoruhusu ushoga.

"Itachukua muda kwa watu wetu kukubaliana na tamaduni za watu wa magharibi, nakumbuka Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron aliwahi kuzungumza sana kuhusu suala hilo na likaleta shida na tafrani kubwa kwa watu wetu," alisema.

"nafikiri kwa watu wetu sidhani kama huu ni muda muafaka wa kujadili suala hilo,hatulitaki na halikubaliki" alisema alipokuwa akihojiwa na mtangazaji wa CNN, Christiane Amanpour.

Amannpour alitaka kujua msimamo wa Rais Kikwete kuhusu haki za mashoga na harakati zinazofanywa ili kuufaya ushoga kama moja ya haki za msingi za binadamu.
Quantity : Add to Cart

1 comment:

  1. Haya mambo yapo na watu wanayafanya kila kukicha, wapo mitaan wapo, magerezani, kila sehemu lakin sijaskia mtu kukamatwa ama kuchukuliwa hatua za kisheria. Wako huru kufanya mambo yao, LAKINI inapotokea kua wanataka sasa hivyo vitendo vyao vitambulike RASMI ama viwe supported na sheria ya nchi, duuh hapo HAPANA

    ReplyDelete

Labels

Blogroll

Labels

About