Welcome to our online store Portal

Template Information

Monday, February 17, 2014

MTWARA - RUVUMA SASA NI LAMI MKATABA WATIWA SAINI LEO


John-Magufuli
Waziri wa Ujenzi, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara itakayotekelezwa katika mikoa ya Ruvuma na Mtwara.
Miradi hiyo itahusisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kati ya Namtumbo na Tunduru ambayo imegawanywa katika sehemi tatu ambazo ni Namtumbo – Kilimasera (km 68.20), Kilimasera – Matemanga (km 58.70) na Matemanga-Tunduru (km 60.70).

Tayari Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ambayo inayofadhili ujenzi huo kwa pamoja na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), imetoa kibali kwa ujenzi wa sehemu mbili za kuanzia Namtumbo hadi Kilimasera na Matemanga hadi Tunduru.  Sehemu kati ya Matemanga na Kilimasera itasubiri kibali kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika ambacho pia kinatarajiwa kutoka hivi karibuni.
Hii ni mara ya pili kwa sehemu hiyo ya barabara kupata makandarasi. Awali kampuni ya Progressive-Higleig Joint Venture kutoka India ndiyo iliyokuwa imeshinda zabuni hiyo mwaka 2010 lakini baadaye ikasimamishwa kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya kimkataba na kuonyesha udhaifu katika utekelezaji wa mradi huo.

Katika hatua nyingine kesho pia utasainiwa mkataba wa ujenzi wa sehemu ya barabara inayoanzia Mangaka mkoani Mtwara hadi Nakapanya (km 70.50) katika mkoa wa Ruvuma. Vile vile utasainiwa mradi mwingine wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kuanzia Nakapanya hadi Tunduru (km 66.50) utakaotekelezwa mkoani Ruvuma.
Kusainiwa kwa miradi hii ni faraja kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Ruvuma pamoja na mikoa yote ya kusini kwani barabara hiyo ni kichocheo kikubwa kwa shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo hayo.
Hafla ya utiaji saini wa miradi hiyo imefanyika leo (Jumatatu) tarehe 17 Februari, 2013 katika Hoteli ya Court Yard (Protea) hapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop