Jehi
la polisi wilaya ya Makete mkoani Njombe linamshikilia Bw. Sadick Sanga
(28) mkazi wa kijiji cha Unyangogo kata ya Iniho wilayani hapa, kwa
tuhuma za kumuua kikatili Bibi Meluti Mbwilo (70) ambaye ni mama yake wa
kambo
Tukio
hilo limetokea Machi 14 mwaka huu ambapo mtuhumiwa alitenda mauaji hayo
kwa kumkatakata na panga kichwani na miguuni wakati marehemu akiwa
jikoni kwake
Akizungumzia
tukio hilo Afisa upelelezi wilaya ya Makete ambaye pia ni kaimu OCD,
Bw. Gosbert Komba amesema kuwa baada ya wananchi kugundua mauaji hayo,
walimkamata mtuhumiwa na kisha wakatoa taarifa kwa jeshi hilo ambapo
walifika mara moja na kumtia mbaroni mtuhumiwa
Amesema
mtuhumiwa alikamatwa na kielelezo ambacho ni panga analodaiwa kulitumia
kutekeleza mauaji hayo na kwa sasa anashikiliwa na jeshi hilo na
atapandishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa kujibu mashitaka
yanayomkabili
Bw.
Komba amekiri vitendo vya mauaji ya kikatili kuendelea kushamiri
wilayani Makete ambapo ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia
sheria mkononi kwani ni kinyume na sheria za nchi
Amesema
mauaji hayo yanahusishwa na imani za kishirikina hivyo, kutokana na
wazee wengi kuonekana wana macho mekundu hivyo watu kuwadhania kuwa ni
wachawi hivyo kuwataka wananchi kuondokana na dhana hiyo potofu
“Unajua
maeneo mengi hapa wilayani watu wanapikia kuni, na kuni zinatoa moshi,
hawatumii gesi ama umeme huko vijijini, hivyo uwezekano wa watu kuwa na
macho mekundu ni mkubwa kutokana na moshi unaotokana na kuni wakati wa
kupika, haimaanishi macho mekundu yao eti ni wachawi” alisema Komba.
0 comments:
Post a Comment