Afisa
Mtendaji MKuu wa Smart Telecom, Afrika Mashariki, Abdullatif Bouziani
akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kwenye
uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Serena,jijini Dar,kulia kwake
ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo,Brian Azecham.
Pazia likishushwa kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kampuni hiyo ya simu za mikononi-Smart.”lets talk.
Afisa
Mtendaji MKuu wa Smart Telecom, Afrika Mashariki, Abdullatif Bouziani
akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari kwenye uzinduzi huo uliofanyika
katika hoteli ya Serena, jijini Dar.
Pichani
kati ni Balozi wa Kampuni hiyo ya simu iliyozinduliwa jijini
Dar,Msanii wa maigizo ya vichekesho atambulikae kwa jina la Hemed
Maliyaga a.k.a Mkwere Orijini akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Smart
Telecom, Afrika Mashariki, Abdullatif Bouziani (shoto) na Afisa Masoko
wa Kampuni hiyo,Brian Azecham wakiwa katika picha ya pamoja.
Viongozi
wakuu wa kampuni ya Smart Telecom, Afrika Masharikii wakiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya washindi waliojipatia zawadi kupitia
mtandao huo,baada ya kushiriki kwenye kampeni ya GIVE US A NAME
iliofanyika hivi karibuni.
IPS kukuza ujasiliamali wa jamii katika mawasiliano ya simu Burundi, Uganda na Tanzania
Shirika
la kuhamasisha viwanda (IPS), chombo na silaha ya maendeleo ya viwanda
chini ya mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Aga Khan (AKFED),jana
wametangaza kuingia katika soko la mawasiliano la Afrika Mashariki chini
ya kampuni iitwayo SMART.
Jina
la kampuni ni matokeo ya kura zilizopigwa Afrika Mashariki katika
kampeni ya Uvumbuzi. Kuzinduliwa kwa kampuni hiyo kutaisaidia AKFED
kukuza huduma zake za kibiashara kwa jamii katika nchi za Burundi,
Tanzania na Uganda, lengo kuu likiwa kuwekeza na kuwahudumia wateja
Mtandao
wa IPS una uwanda/uelewa mpana katika sekta ya mawasiliano. Ni
washirika wakubwa wa Roshan shirika linaloongoza katika utoaji wa huduma
za mawasiliano nchini Afghanistan na pia washirika muhimu katika
shirika la Tcell linaloongoza katika kutoa huduma Tajikistan.
IPS
pia ni wawekezaji wakubwa na wa pekee waliowekeza SEACOM submarine
cable venture in East Africa. Wakati umefika ambao ushirika wa IPS ndani
ya SMART utaleta ushirikiano na kuweka record ya ushirikiano wa
makampuni ya simu Nepal na Cambodia na kuwafanya wawe waongozaji katika
soko hili.
Kuzinduliwa
kwa SMART kutashirikisha uzoefu wa AKDEF katika kuwekeza kwa lengo la
kuhamasisha ujasiliamali na ujenzi wa uchumi wa sauti ambao utatoa fursa
nyingi za ajira na kuboresha maisha ya watu. Afrika Mashariki. AKFED
imewekeza Serena Hotels, Diamond Trust Bank, Jubilee Insurance Group,
National Media Group na katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji na
miundombinu kama vituo vya nguvu ya umeme vya Bujagali na Tsavo.
“Kazi
zetu katika mawasiliano kwa njia ya simu hasa Roshan-Asia ya kati ni
kuboresha uwekezaji wa jamii katika miundombinu ya jamii, huduma za afya
na elimu. Pia kutengeneza biashara yenye mafanikio katika soko ili
tuweze kujitofautisha na washindani wengine, Tunatazamia kuwa uwekezaji
katika kampuni dada ya AKDN utakua umeenea katika nchi za Burundi,
Tanzania na Uganda kwa zaidi ya miaka 100” alisema Lutaf Kassam Meneja
wa IPS
SMART
itaingia katika masoko haya ikiwa na dhamira ya embrance tamaduni za
ndani ili kuboresha jamii wanakofanyia kazi.mfano mzuri wa dhamiri hii
ni njia ambayo jina la kampuni lilivyochaguliwa. Kampeni ya Tupe Jina
ilizinduliwa mwishoni mwa mwaka 2013 ikiwahamasisha watu wa Afrika
Mashariki kupendekeza na kulipigia kura jina la kampuni.
Kampeni
hiyo iliwavutia zaidi ya watu 70,000 na majina tofautitofauti
yalipendekezwa na kupigiwa kura. Mwisho kampeni ililipata jina la SMART
ikikusudia kuangalia uvumbuzi wa mawazo katika soko la Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment