Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma.
Suala
la Jinsia katika uongozi wa Bunge Maalum la Katiba limeibua Mjadala
mzito katika nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa bunge hilo.
Mjumbe
wa Bunge hilo Lediana Mung’ong’o ndiye aliyekuwa wa kwanza kuibua suala
hilo wakati wa mjadala kuhusu marekebisho ya kanuni za bunge kipengele
8(i) kinachozungumzia utaratibu wa kumchagua Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti.
Mung’ong’o
alitaka kipengele hicho kuzingatia uhusiano wa kijinsia, ambapo kama
mwenyekiti atakuwa ni mwanaume, makamu wake awe mwanamke au kama
Mwenyekiti atakuwa mwanamke, makamu wake awe mwanaume.
“Mwenyekiti
hili suala la Mwenyekiti na Makamu wake hatuna budi kuangalia suala la
jinsia kwamba ikiwa mwenyekiti atakuwa ni mwanaume, makamu wake awe
mwanamke au kama Mwenyekiti atakuwa mwanamke, makamu wake awe mwanaume”
amesema Mung’ong’o.
Naye
Mjumbe wa Bunge hilo Anna Abdalah amesema kuwa suala hilo lilikosewa
Tangu awali hivyo hakuna budi makubaliano yafanyike kwa busara maana
wanawake wenye sifa na uwezo wapo wengi Tanzania Bara na Zanzibar.
Akichangia
katika suala hilo Mjumbe wa Bunge Hilo ambaye ni Naibu Waziri Wizara ya
Fedha Adam Malima amesema kuwa ili kuwepo kwa amani na Mshikamano
sheria haina budi kusema wazi endapo Mwenyekiti atatoka Tanzania Bara
basi Makamu wake atoke Zanzibar.
Akijibu
hoja hiyo Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman amesema
kuwa suala hilo liwe la marekebisho lakini si kwa kuvunja sheria hiyo.
“Sharti
hilo likibadilishwa litakuwa ni kituko na tutakuwa tunarekebisha sheria
ambazo hazikutungwa na Bunge Maalum la Katiba hivyo ni busara kufanya
makubaliano ili kufikia muafaka wa jambo hilo” amesemaOthman Masoud
Othman.
0 comments:
Post a Comment