Afisa Mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) akiongea katka uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus, ambapo jana washiriki wapatao 29 waliingia kijijini kuanza kukabiliana na changamoto za kuweza kupata shilingi milioni 25 za kitanzania.
Wageni waalikwa waliofika kijijini cha Maisha Plus kuangalia uzinduzi…
Washiriki wa shindano la Mshindi wa Maisha Plus wakipewa maelekezo machache mara baada ya kuwasili kijijini kwao.
Mmoja ya wawakilishi toka Oxfam ambao ni wadhamnini wa Maisha Plus 2014 akizungumza machache. Pembeni yake ni Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya).
Mkuu wa Kijiji… Mwite babu wa kaya akiwepo kuhakikisha wanakijiji wanakaribishwa kwa shangwe.
Wageni waalikwa.
Kazi ya kujenga nyumba za kuishi washirki wa maisha plus ikiendelea… ambapo washiriki hao walitakiwa kujenga nyumba zao za kuishi ndani ya masaa 48.
Kila mmoja anawajibika kuhakikisha kazi ya kujenga nyumba inafanikiwa.
Wadau kutoka Oxfam wakibadilisha mawazo mara baada ya kufika katika tukio la uzinduzi wa wawashiriki kuingia kijijini.
6
Safari ya kuelekea kijiji cha Maisha Plus imeanza rasmi… washiriki wakiwa wamebeba mabegi yao ambapo kila mmoja alibeba mzigo wake mwenyewe kwa kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 1.5
Safari ikiendelea huku washiriki wakiwa wameshachoka… wengine walitamani kughairi kuendelea na safari.
Wengine ilibidi wasaidiane kupeba mizigo.
Hakuna kuchoka, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe…
Wengine waliamua kulala ili waweze kunyoosha mgongo.