Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akitia saini
hati ya makubaliano ya msaada wenye thamani ya ziadi ya bilioni 6
unaolenga kukuza sekta ya kilimo uliotolewa na Serikali ya Japan
kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA) leo jijini Dar es salaam.
Kulia ni Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto)
akikabidilishana nakala ya makubaliano waliosainina na Balozi wa Japan
nchini Masaki Okanda (kulia) ambayo yanahusu msaada uliotolewa na
Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA) leo
jijini Dar es salaam.
Mwakilishi
wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi akikabidilishana nakala za
mkataba uliosainiwa na Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia) na
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) leo
jijini Dar es salaam.
Balozi
wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia), akiteta jambo na Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) baada ya Serikali ya
Tanzania kusaini mkataba na Serikali ya Japan leo jijini Dar es
salaam.
Serikali
ya Tanzania imepokea msaada wa zaidi ya sh. bilioni sita (6) za
Kitanzania ambazo ni sawa na Yen milioni 380 zilizotolewa na Serikali ya
Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa la Misaada (JAICA) .
Kauli
hiyo ilitolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Dkt. Servacius Likwelile wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa kupokea
msaada huo ambao utatumika kukuza sekta ya kilimo na kupunguza
umasikini nchini.
Katibu
Mkuu Dkt. Likwelile alisema kuwa msaasa huo utatumika kununulia mbolea
(UREA) ili kuongeza tija katika uzalishaji mazao na unalenga kuwafikia
wakulima wadogo wadogo nchini ili kuwaongezea kipato chao.
Katibu
Mkuu huyo alisema kuwa msaada huo umekuja muda muafaka ambapo serikali
inachukua hutua za makusudi kuinua sekta ya kilimo ambayo inawaajiri
watanzania takribani asilimia 74 nchini.
Aidha,
Katibu Mkuu aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaaada huo na
kumhakikishia Balozi wa Japan nchini Mh. Masaki Okanda kuwa msaada
uliotolewa na Japan kupitia JAICA utatumika kulinganana malengo
yaliyokusudiwa.
Kwa
upande wake Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda alisema kuwa msaada
uliotolewa na Serikali yake kupitia JAICA unalenga zaidi sekta ya kilimo
na kusaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara na masoko ambayo ndiyo
kiini cha ufanisi katika sekta hiyo.
Naye
Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi alisema kuwa
mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Japan ni wa kihistoria
ulianzishwa tangu mwakqa 1974 ambapo mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa
unanufaika na misaada hiyo katika kuboresha kilimo.
Akimshukuru
Katibu Mkuu Likwalile na Balozi wa Japan nchini Okanda, Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Yamungu Kayandabila alisema
kuwa amefurahi Wizara yake kupata masaada huo na ameahidi kuwa utatumika
kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta kilimo chenye tija nchini.
Serikali
ya Japan nchini kwa kushikiana na Tanzania katika kusimamaia kilimo
inaongozwa na nguzo kuu tatu ambazo ni kilimo, miundombinu na utawala
bora, hali ambayo itaihakikishia nchi kuwa na uhakika wa mazao bora na
hivyo kupunguza umasikini nchini.
0 comments:
Post a Comment