Mwenyekiti
wa Timu ya watoto wa mitaani ya jijini Mwanza Alfat Mansoor (Dogo)
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya timu hiyo kuwasili
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jijini Dar es
Salaam.
Mchezaji
aliyesabibisha timu ya watoto wa mitaani kutoka Tanzania kuibuka
mabingwa wa Dunia kw kufunga magoli matatu kwa mojadhidi ya Burundi
Frank William(mwenye kofia nyekundu) akiwa na baadhi ya wachezaji
wenzake mara baada ya juwasili airport,kushoto ni Hassan Jaffar,Emmanuel
Amos, na Hassan Seleman.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yassoda akiwa amebeba
kombe la ubingwa dunia mara baada ya kupokea timu ya watoto wa mitaani
kutoka Tanzania iliyochukua ubingwa huo kwa kuifunga timu kutoka Burundi
jumla ya magoli 3-0. Timu hiyo imewasili nchini jana majira ya saa 9:35
mchana na kulakiwa na uongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa soka.
Wachezaji
wa timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania ilyo nyakuwa ubingwa wa dunia
katika mashindano yaliyofanyika nchini Brazil kwa kushirikisha timu za
watoto wa mitaani, wakiwa wamebeba makombe waliyoyapa katika mashindano
hayo.
Afisa
Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bw. Frank Shija akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wachezaji wa timu ya watoto wa mitaani(Picha zote na Frank Shija, Afisa
Mawasiliano Serikalini, WHVUM).
0 comments:
Post a Comment