Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya Wananchi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika Mei 16, 2014 katika viwanja vya Mwananchi
Squire mjini Urambo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani
ya CCM, kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia ya
kuzitatua katika mkoa wa Tabora.
Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Kinana kwenye mkutano huo.
Kinana akiinuliwa baada ya kusimikwa uchifu wa Wanyamwezi kabla ya kuhutubia mkutano huo.
Kinana akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kijadi waliomtawaza kuwa chifu wa Wanyanyembe.
Kaibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisiitiza jambo akihutubia
maelfu ya Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mei 16, 2014
katika viwanja vya Mwananchi Squire mjini Urambo, akiwa na Kinana katika
ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za
wananchi huku akijadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoa wa Tabora.
Mbunge wa Urambo Samwel Sitta akihutubia wananchi kwenye mkutano huo.
Kinana
akimvisha kofia ya usalama, Katibu wa CCM kata ya Kondamoyo,
Barakabraka wakati akimkabidhi pikipiki . Jumla ya pikipiki 16
zimetolewa na Sitta na Mama Sitta
Katibu
wa CCM tawi la Boma Village Fatuma Ulaya akikabidhiwa baiskeli na
Kinana, ikiwa ni miongoni mwa basikeli 96 walizokabidhiwa Makatibu wa
matawi kutoka kwa Samwel Sitta wakati wa mkutano huo.
Makatibu wakiwa na baaiskeli zao baada ya kukabidhiwa na Kinana kwenye mkutano huo.
Vijana wakiwa wamedandia kwenye lori lililokuwa limeegeshwa ili wapate kumuona vizuri Kinana kwenye mkutano huo.
Kinana
akizindua mradi wa Kina mama wa mashine ya kukamua alizeti, kijiji cha
Itundu wilayani Urambo akiwa katika ziara hiyo ya mkoa wa Tabora.
Kinana Sitaa wakishiriki ujenzi shule ya sekondari Uyumbi, Urambo.
Mnara uliopo kwenye shamba la kituo cha kilimo cha Umwagiliaji wa matone.
Kinana akiangalia mhindi kwenye shamba darasa la kilimo cha mwagiliaji kwa matone la Kapilula, Urambo.
Kinana akitazama mahindi yanavyopata maji kupitia matone, katika shamba darasa la Kapilula, Urambo.
Mbunge wa Viti Maalum Mama Margareth Sitta akitazama mahindi yalivyozaa kwenye shamba hilo.
Kinana katika wodi ya wazazi ya Yuwilindila.
Muuguzi Mkunga wa Zahanati ya Izenga, Urambo mkoani Tabora, akimuonyesha Kinana hifadhi ya dawa.
Vijana wa Chipukizi wakimchezea paredi maalum Kinana wakati wa mapokezi eneo la Zimbili, Urambo.
Kinana akipita katika Vijana wa CCM wakati wa mapokezi eneo la Zimbili, Urambo.
Kinana akilakiana kwa shangwe na Sitta wakati wa mapokezi yake katika kijiji cha Izimbili, Urambo.
Madiwani
kwa tiketi ya CUF, Kandola Nyanda (Kata ya Nsenda) na Kadada Mohamed
kutoka Kata ya Usoke ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya
na Maji katika Halmashauri ya Urambo (Wapili kushoto), wakimsalimia kwa
furaha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, wakati wa mapokezi yake
yaliyofanyika Kijiji cha Izimbili Kata ya Usoke, akiingia wilaya ya
Urambo kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na
kusikiliza kero za wananchi huku akijadiliana nao njia ya kuzitatua
kero hizo mkoani Tabora.
Kinana na Nape wakisalimia baada ya kukagua Zahanati ya Izengabatogwile.
Kinana
na Nape wakisalimia sungusungu wilayani Urambo mkoani Tabora baada ya
sungusungu hao kupokea msafara wa Kinana.
0 comments:
Post a Comment