Ukuaji
endelevu wa uchumi wa Tanzania umeona ongezeko la kampuni za nje
zikiingia nchini zikiwa na nia ya kuzindua bidhaa au huduma zao kwa
Watanzania walio wengi. Mafanikio kwa bidhaa na huduma hizi yanategemea
mambo mengi kuanzia mazingira hadi uhitaji, kuonyesha kwamba
zinakubalika katika soko.
Kampuni
moja ambayo imeona mafanikio yaliotulia na kua mtoa huduma tegemezi kwa
Watanzania, ni kampuni ya vifaa vya umeme ya Samsung. Kupitia bidhaa
zao mbalimbali wameshuhudia mauzo ya zaidi ya bidhaa zao 50,000 ndani ya
mwaka mmoja. Katika mwaka ambao unatarajiwa kua wa mafanikio kwa
kampuni hii Wanatazamia kudaka asilimia 30 ya soko la vifaa vya
kielektroniki.
Takwimu
hii inaweza kuja kama mshangao lakini ikiwekwa kwenye mtazamo halisi
inajenga picha yenye uwazi. Mafanikio haya yanatokana na utafiti katika
soko la Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla. Ukichanganya mambo kama
vile uhitaji wa vifaa vinavyo okoa gharama na zenye uwezo wa kuhimili
mazingira ya Kiafrika. Kampuni ya Samsung imeendelea kua mbele kutokana
na ubunifu wa bidhaa ambazo kwa pamoja zajulikana kama “Built for
Africa”. Sehemu ya friji ndio inazidi kupendwa na wateja wengi katika
miaka michache iliopita kutokana na kuaminika na uwezo wa kuhimili
mazingira ya Kiafrika. Katika kujengea mafanikio hayo, Samsung
inaangalia kulenga soko kupitia aina mpya za friza zinazofaa kwa
matumizi ya nyumbani na biashara. Uhitaji wa kuwa tofauti na asili ya
uongozi ndio inaweka jina sokoni mpaka sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania Bw. Dongha Jang aliunga mkono kauli zilizotajwa alipohojiwa na kusema “Samsung
daima inatafuta kuunganisha wateja wake na bidhaa zake kwa kutoa bidhaa
zinazosaidia kustawisha maisha ya mtumiaji. Sisi lengo letu ni kuleta
teknolojia ya kisasa katika mfumo ambao ni muhimu zaidi kwa soko la
Tanzania.” Mr. Jang alifafanua zaidi kuhusu uzinduzi wa bidhaa kadha moja kwa moja kwenye soko la Tanzania “katika
hiki kipindi cha miaka michache iliopita tumeona umuhimu wa kuleta
bidhaa mpya moja kwa moja kwa watumiaji wetu wa Tanzania kuliko
kutegemea uzinduzi kwenye soko la kimataifa”. Miongoni mwa
bidhaa Bw. Jang alizokuwa anaongelea katika msemo wake ni uzinduzi
sambamba wa bidhaa mbili muhimu za nyumbani ambazo ni Samsung Duracool
freezer na Triangle AC.
Uzinduzi
huo ulikuwa sehemu ya mkakati wa kudumisha nafasi ya Samsung kama
kiongozi wa vifaa vya umeme katika majumba ya Watanzania. Samsung
Duracool freezer na Triangle AC zina sifa zinazoruhusu ufanyaji kazi kwa
kiwango cha juu ukizingatia mazingira magumu ya Tanzania ikiwemo
usambazaji wa umeme usioaminika na gharama zinazo panda. Samsung
wanakuja na ahadi ya kurahisisha maisha kwa kuwa na bidha zenye gharama
nafuu kwa mtumiaji.
Katika
soko ambalo halitabiriki kama la Tanzania, kampuni hii ya vifaa vya
umeme imeweza kutambua maeneo yaliokuwa ya maslahi kwa wateja wake
kimahesabu. Hii ni dhahiri leo kupitia uwepo wake katika mitaa
mbalimbali nchini. Katika mazingira ambayo hayana uhakika wa mafanikio
kwa wote, Samsung inaendelea kushinikiza mipaka ya ubunifuu wa bidhaa
ambazo “zimetengenezwa kwa ajili ya Africa”.
0 comments:
Post a Comment