Kuna kila dalili kuwa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na zile za Kamati za Bunge zinazosimamia fedha za umma, huenda zikawang’oa baadhi ya mawaziri.
Hofu kuu inaonekana kuwakumba baadhi ya mawaziri
huku waziri mmoja mwandamizi aliyezungumza na gazeti hili akisema;
“Wengi wetu tumeshikwa na kihoro, hatujui nini kitatokea.”
Ni ripoti za aina hiyo zilizowasilishwa bungeni
Aprili 2012, zilisababisha kuwapo shinikizo kwa Rais Jakaya Kikwete
kupangua baraza lake la mawaziri, Mei 4, 2012 na kuwatupa nje mawaziri
hao.
Katika panguapangua hiyo, Rais Kikwete aliwatosa
mawaziri sita akiwemo Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo na Waziri wa
Viwanda, Biashara na Masoko na Mbunge wa Moshi Vijijini,Dk Cyril Chami.
Wengine waliotoswa kwa shinikizo hilo la wabunge
ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri wa Nishati na
Madini, William Ngeleja na Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu.
Pia Naibu Waziri wa Uchukuzi wa wakati huo,
Athuman Mfutakamba alitoswa sanjari na Waziri wa Afya, Dk Haji Mponda na
Naibu wake, Dk Lucy Nkya.
Katika mkutano huu wa 14 unaoendelea, zipo tetesi
kuwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamejipanga kuwang’oa
mawaziri kamili sita na manaibu mawaziri saba kwa kushindwa kuwajibika.
“Hizi siku nne za taarifa za kamati, inawatia
kiwewe baadhi ya mawaziri na hakuna ubishi ripoti hizi zinaweza
kuchochea kuwapo uamuzi mgumu,” alidokeza mmoja wa mawaziri waandamizi.
Mbunge wa Ubungo na Mkurugenzi wa Habari wa
Chadema, John Mnyika, alisema pia kila waziri kivuli wa wizara ambayo
imeonekana kuongozwa na waziri mzigo, amepewa maelekezo maalumu.
0 comments:
Post a Comment