Mkurugenzi
wa TEHAMA wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ally
Simba akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa
Patrick Makungu (hayupo pichani) katika ufunguzi wa kongamano la siku
mbili kuhusu sheria ya mtandao jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick
Makungu akifafanua jambo wakati akifungua kongamano la siku mbili kuhusu
sheria ya mtandao ambalo limeshirikisha wadau mbalimbali wa mtandao,
kongamano hilo limefanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wadau wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick Makungu (hayupo
pichani) wakati akifungua kongamano la siku mbili kuhusu sheria ya
mtandao jijini Dar es Salaam.
Mtoa
mada wa kwanza katika kongamano la siku mbili kuhusu sheria ya mtandao
Bw. Said Kalunde akitoa mada iliyohusu uhalifu wa mtandao jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini kongamano la siku mbili
kuhusu sheria ya mtandao jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Eliphace
Marwa – Maelezo).
Serikali
yaendelea kushirikisha wadau mbalimbali wa mitandao ili kuweza kupata
sheria itakayosimamia matumizi salama ya mitandao hapa nchini.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kongamano la siku mbili jijini Dar es Salaam
mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Profesa Patrick Makungu alisema kuwa serikali inashirikiana na wadau
mbalimbali nchini na nje ya nchi kwa lengo la kupata maoni yao.
“Kongamano
hili linakutanisha wadau muhimu ambao maoni yao yataweza kufanikisha
kupatikana kwa sheria ya mtandao ambayo itakuwa ndiyo suluhisho la
uhalifu wa mtandao ambao unaonekana kushamiri sana hapa nchini na
duniani kwa ujumla,” alisema Profesa Makungu.
Aidha
Profesa Makungu aliongeza kuwa katika kupambana na uhalifu wa mtandao
Tanzania imeandaa miswada mitatu ya sheria ya usalama wa mtandao ambayo
pia inatumika katika Shirikisho la Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC).
“Sheria
hizo ni sheria ya mtandao, sheria ya usalama wa taarifa na sheria ya
biashara mtandao kwa kufanya hivi tuko sambamba na Jumuiya ya afrika
Mashariki, Shirikisho la Maendeleo Kusini mwa Afrika na Umoja wa Afrika
ambao wote wana lengo moja la kupambana na uhalifu wa mtandao,”
aliongeza Profesa Makungu.
Naye
Mkurugenzi wa TEHAMA toka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Dkt. Ally Simba alisema kuwa kama hakuna sheria ya mtandao ni rahisi
uhalifu wa mtandao kupunguza wawekezaji kwani usalama wa fedha unakuwa
ni mdogo.
Serikali
inaendelea kukusanya maoni ya wadau mbalimbali kuhusu sheria ya
mtandao kwani mchakato wa kupata sheria uko katika hatua za mwisho na
ambapo mwakani katika miezi ya mwanzoni sheria hii itakuwa tayari.
0 comments:
Post a Comment