: Yasema itatafakari na kuamua ipasavyo hoja za Tume
:Yasisitiza mchakato utumike kuwaunganisha Watanzania
Chama
Cha Mapinduzi kimeipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi
iliyofanya kuufikisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya hapa
ulipofika. Akizungumza katika mahojiano maalumu na baadhi ya waandishi
wa habari mara baada ya Tume kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba Nape
alisema;
“CCM
inaipongeza Tume kwa kazi waliofanya, tunatambua kazi kubwa
waliyofanya, wamekamilisha kazi waliyotumwa salama na kwa wakati. Sasa
tuwaachie wanaondelea na mchakato yaani bunge la katiba na hatimaye
wananchi. Tunautakia kila lakheri mchakato huu, utumike kutuunganisha
watanzania badala ya kutugawa” amesema Nape
Kuhusu pendekezo la Tume la muundo wa Muungano wa serikali tatu Nape anasema;
“Tumesikiliza
hoja za tume juu ya sababu za kuendelea kupendekeza muundo wa serikali
tatu, tumezisikia, tutazichukua,kuzipeleka kwenye vikao vya Chama baada
ya tafakuri ya kutosha tutaamua ipasavyo” alisisitiza Nape.
Aidha Nape alitumia nafasi hiyo kuwatakia watanzania kila lakheri kwenye mwaka mpya wa 2014.
0 comments:
Post a Comment