Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji John Utamwa
baada ya kupokea maombi ya Zitto kupitia kwa Wakili wake, Albert Msando
kutaka rufaa yake aliyoiwasilisha Baraza Kuu kusikilizwa kwanza kabla ya
kufanyika uamuzi mwingine.
Kamati Kuu ya chama hicho, ilipanga kukutana leo
ikiwa na ajenda kuu tatu; kupanga mpangokazi wa chama kwa mwaka 2014,
kupokea utetezi wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali
zilizoelekezwa
Zuio hilo lilikuja pia baada ya kutupiliwa mbali
maombi ya pingamizi la Chadema lililowasilishwa na Mkurugenzi wa Katiba
na Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Peter Kibatala.
Akizungumza jana baada ya uamuzi huo wa Mahakama,
Mwanasheria Mkuu Chadema, Tundu Lissu alisema hakuna jinsi zaidi ya
kukubaliana na uamuzi huo... “Tumekubali kutokumjadili Zitto lakini
tuliomba Mahakama iruhusu kuhojiwa kwa Dk Kitila Mkumbo na Samson
Mwigamba.
Zitto alifungua kesi Mahakama Kuu akiiomba iizuie
Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Katibu Mkuu pamoja na Kamati Kuu ya
Chadema kumjadili, kumchukulia hatua yoyote kuhusu uanachama wake hadi
hapo rufaa yake aliyoikata Baraza Kuu la Chadema itakaposikilizwa.
Pia katika maombi yake, Zitto alitaka Mahakama
kuzuia kwa njia yoyote, Kamati Kuu kumwingilia katika utekelezaji wa
majukumu yake ya Ubunge wa Kigoma Kaskazini.
Mbali na ombi hilo, pia aliiomba Mahakama
kumwamuru Katibu Mkuu wa Chadema ampatie nakala ya mashtaka na maelezo
ya uamuzi uliofikiwa na Kamati Kuu Novemba 22, 2013 wa kumwondolea
nyadhifa zake ili aweze kuwasilisha rufaa yake Baraza Kuu la Chadema
kupinga uamuzi huo.
Zitto kupitia wakili wake, Msando alifungua kesi
hiyo ya madai namba moja ya mwaka 2014 akipinga uamuzi huo wa Novemba
22, 2013 pamoja na hatua zaidi zilizoagizwa kuchukuliwa dhidi yake
kuhusiana na uanachama katika chama chake. Walalamikiwa ni Bodi ya
Wadhamini na Katibu Mkuu wa Chadema.
Walalamikiwa hao, kupitia kwa Lissu na Kibatala
waliwasilisha pingamizi wakiiomba Mahakama itupilie mbali kesi hiyo kwa
madai kuwa vifungu vilivyotumiwa katika kuwasilisha maombi hayo havikuwa
sahihi.
Pia waliomba Mahakama hiyo kutupilia mbali kesi
hiyo kwa madai kuwa hati ya kiapo iliyotumiwa kuwasilisha maombi hayo
ina upungufu wa kisheria na kwamba Mahakama hiyo haina uwezo wa
kuyasikiliza.
Zitto kupitia Wakili Msando, alisisitiza kuiomba Mahakama hiyo
kuamuru Kamati Kuu ya Chadema na uongozi wowote wa chama hicho
kutokuingilia, kujadili au kuchunguza suala lolote la uanachama wake
hadi hapo rufaa yake itakapopitiwa na Baraza Kuu la Chadema.
Alisema bado ni Mbunge halali wa Kigoma Kaskazini
na aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama hicho hadi Novemba
22, 2013, Kamati Kuu ya Chadema ilipoamuru avuliwe nyadhifa zote
alizokuwa nazo na kuagiza hatua zaidi zichukuliwe kuhusiana na uanachama
wake. Uamuzi huo uliwasilishwa kwake kwa maandishi kupitia kwa
Mkurugenzi wa Habari wa Chadema, John Mnyika na Lissu alipozungumza na
vyombo vya habari Novemba 26, 2013 alitangaza madai yao kisha kutoa siku
14 kwa watuhumiwa kujibu hoja zao.
Akizungumza jana, Dk Kitila Mkumbo alisema
amejiandaa kisaikolojia na ana subiri kwenda kwenye kikao hicho
kusikiliza na kujibu maswali yoyote atakayoulizwa kwa kuwa huo siyo
mtihani ambao anatakiwa kujiandaa kabla ya kwenda kuufanya.
Alipoulizwa kama amejiandaa kupokea uamuzi wowote
utakaotolewa, Mkumbo alisema: “Suala kwamba haki itatendeka au la,
nitalizungumza nikitoka kwenye kikao.”
Kwa upande wake, Samson Mwigamba alisema ana
uhakika kuwa haki haitatendeka kwa sababu haikutendeka tangu mwanzo
alipowasilisha malalamiko yake kwenye kamati hiyo.
“Haki haiwezi kutendeka, wakati ule nilikata rufaa, badala ya kuijadili, walinivua uongozi,” alisema Mwigamba.
Baraza la Uongozi la Chadema Wilaya ya Tanga,
limemvua wadhifa Katibu wa Wilaya hiyo, Khalid Rashid kwa makosa 10
likiwamo la kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kumvua madaraka
Zitto. Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tanga, Said Mbweto, alisema Khalid
amekosa sifa za kuwa Katibu wa Wilaya.
Aliyataja baadhi ya makosa yake kuwa ni kulivunjia
heshima Baraza la Wazee wa Mkoa, kwenda Pangani kufanya mkutano kinyume
na sheria, kupinga kufukuzwa kwa Zitto, kuandika barua ya dharau kwa
uongozi wa Chadema Mkoa na kukusanya saini za wanachama kwa kisingizio
kuwa ni agizo la Chadema Taifa.
0 comments:
Post a Comment