Mkurugenzi
Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waandishi wa
habari(hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya utoaji mikopo kwa mwaka wa
masomo 2014/2015, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi.
Zamaradi Kawawa.
Baadhi
ya Waaandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu
na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw.
Cosmas Mwaisobwa wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Serikali
imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na masomo ya
stashahada maalum ya ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Elimu na Mawasiliano toka
Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati
wa Mkutano na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam.
“
Wanafunzi wapatao 5,000 wanatarajiwa kujiunga na stashahada maalum
katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo wote watanufaika na mikopo ya
elimu ya Juu.”Alisema Mwaisobwa
Akifafanunua, Mwaisobwa alisema kuwa lengo la mpango huo ni kusaidia kuondoa tatizo la walimu wa masomo ya sayansi hapa nchini .
Aidha
Mwaisobwa alibainisha kuwa jumla ya maombi 58,037 ya mikopo yalikuwa
yamepokelewa hadi kufikia Julai 2014 ambapo maombi 37,689 ni waombaji wa
kiume na 19,592 ni waombaji wa kike.
Pia
Mwaisobwa alibainisha kuwa majina ya wanafunzi watakaopata mikopo
kulingana na udahili yatatangazwa kwenye tovuti ya Bodi ambayo ni www.heslb.go.tz .na taarifa hiyo itatangazwa katika vyombo vya habari.
Bodi
ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) inakusanya wastani wa
shilingi bilioni 3 kwa mwezi ikiwa ni marejesho ya mikopo iliyokwisha
tolewa.
0 comments:
Post a Comment