Welcome to our online store Portal

Template Information

New Products
Showing posts with label Bungeni. Show all posts
Showing posts with label Bungeni. Show all posts

Saturday, May 17, 2014

KUMEKUCHA BUNGENI


PG4A9520
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Naibu wake, Pereira Sirima (kulia) wakipongezwa na Wabunge baada ya bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo, bungeni mjini Dodoma May 16, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
PG4A9513
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William  Lukuvi, bungeni mjini Dodoma.
PG4A9525
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Makambako, Deo Sanga (kushoto) na Mbunge wa Viti Maaliam, Lediana Mng’ong’o bungeni mjini Dodoma.

View detail

Saturday, December 21, 2013

RIPOTI YA MH. SAID NKUMBA ILIYOSABABISHA MAWAZIRI WANNE KUACHIA NYAZFA ZAO

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Ripoti ya Mh. Said Nkumba jinsi ilivyozua kizaazaa jana bungeni mjini Dodoma, watanzania wengi wameisifu ripoti hiyo kwa kuibua maovu mengi ktk oparesheni hiyo, kwa kuisoma ripoti yote Bofya hapa View detail

HOTUBA YA WAZIRI MKUU BUNGENI LEO TAR 21/12/2013 KUFUNGA MKUTANO WA 14 WA BUNGE


I:          UTANGULIZI 
a)          Masuala ya Jumla

Mheshimiwa Spika,
1.            Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo. Tumekuwepo hapa Dodoma kwa takriban siku 15 za kazi ambapo tumeweza kutekeleza majukumu na kazi za Mkutano wa 14 wa Bunge lako Tukufu ambapo tunahitimisha shughuli zilizopangwa hivi leo.

Mheshimiwa Spika,
2.            Nitumie nafasi hii ya mwanzo kabisa kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Asha Rose Migiro, (Mb.) kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Mbunge katika Bunge lako Tukufu.  Wengi wetu tunafahamu uwezo mkubwa wa Dkt. Asha Rose Migiro na bila shaka ndiyo sababu Mheshimiwa Rais alifanya uamuzi wa kumteua kuwa Mbunge kwa kuzingatia sifa nzuri alizonazo. Pamoja na kumpongeza napenda kumtakia kazi njema ndani na nje ya Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika,
3.            Tangu Mkutano wa 13 wa Bunge baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wamepotelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki.  Napenda kutumia fursa hii kuwapa pole wote waliofikwa na misiba hiyo. Lakini katika Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge walipata fursa ya kujadili Azimio la Bunge kuhusu kuungana na Nchi ya Afrika Kusini, katika kuombeleza kifo cha Muasisi, Mpinga ubaguzi wa rangi, Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Madiba Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba 2013.  Wote tunakubaliana kwamba huu ni msiba Mkubwa kwa Dunia nzima na hasa kwa wale wanaomfahamu Mzee Mandela na historia yake. 


View detail

KILICHOWAKUMBA MAWAZIRI WANNE NCHINI TANZANIA HIKI HAPA

waziri mkuu mizengo Pinda akijibu masualili leo bungeni
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
 Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amethibitisha hayo jana jioni Bungeni mjini Dodoma.
Mawaziri hao waliotenguliwa nyadhifa zao ni: Mhe. David Mathayo David wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki wa Maliasili na Utalii, Mhe. Emmanuel Nchimbi wa Mambo ya Ndani na Mhe. Shamsi Vuai Nahodha wa Ulinzi.
Mhe. Kagasheki alitangaza kujiuzulu mapema kabla uamuzi huo uliotangazwa na Waziri Mkuu.

Hizi ni baadhi ya post kwenye wall ya  Facebook ya Mh Zitto Kabwe kufuatia kusomwa kwa Taarifa ya Kamati ya BUNGE kuhusu Operesheni Tokomeza.
Untitled
Untitled 1
Untitled 2
Untitled 3

View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop