Welcome to our online store Portal

Template Information

New Products
Showing posts with label polisi. Show all posts
Showing posts with label polisi. Show all posts

Friday, January 17, 2014

POLISI WADAIWA KUUA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Polisi wilayani Kaliua, inadaiwa kumuua mtu mmoja na kumjeruhi mwingine baada ya wananchi zaidi ya 200 kuvamia kituo kidogo cha polisi kwa lengo la kumtoa mtuhumiwa ili wajichukulie sheria mkononi.
Tukio hilo limetokea baada ya wananchi wa Kijiji cha King’wangoko, Kata ya Sasu kuvamia kutaka kumdhuru Shija Matenga, anayetuhumiwa kuiba ng’ombe watano Kasulu, Kigoma.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Peter Ouma, akielezea tukio hilo alisema Mkuu wa Kituo Kidogo cha King’wangoko, Sajenti Kimola alipokea simu kutoka kwa Wakala wa Mnada wa Konanne, kuwa wananchi wamemkamata na wanataka kumuua.
Kutokana na hali hiyo, Sajenti Kimola alituma askari wawili wakiwa na silaha na kumwokoa mtuhumiwa na kuanza kuondoka naye kitendo kilichokasirikiwa na wananchi walioanza kurusha mawe na fimbo ili kuwazuia askari wasimpeleke kituoni hali hiyo ilichosababisha askari kupiga risasi hewani kuwatawanya wananchi.
“Askari walitumwa walifanikiwa kumwokoa mtuhumiwa jambo ambalo liliwachukiza wananchi waliotupa mawe na fimbo ili kuwazuia askari wasiondoke na mtuhumiwa ambao walilazimika kufyatua risasi hewani kuwatawanya,”alisema Ouma.
Kwa mujibu wa Kamanda Ouma, baada ya askari kumfikisha mtuhumiwa kituoni na kumfungia mahabusu, wananchi walifuatilia na kufika kituoni alipo mtuhumiwa na kushinikiza atolewe.
Alisema askari walipoona wananchi wanataka kutumia nguvu walifyatua risasi hewani kuwatawanya na bahati mbaya risasi moja ilimpata John Joseph bega la kulia kufariki papohapo.
Mwingine aitwaye Malembeka Matemele alijeruhiwa kwenye paja la mguu wa kulia na amelazwa Hospitali ya Wilaya ya Urambo. kwa matibabu.
View detail

Thursday, December 19, 2013

JESHI LA POLISI LATAKIWA KUONGEZA USHIRIKIANO NA OFISI YA MKURUGENZI WA MASHTAKA

  036
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na  Kamishna Mpya wa Polisi Zanzibar  Bwana Hamdan Omar Makame aliyefika Ofisini kwake katika jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mbweni kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
060
Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame akibadilishana mawazo na Mamaku wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ofisini kwake Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
(Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ).

JESHI la Polisi Nchini limetakiwa kuongeza ushirikiano wa karibu zaidi na Ofisi ya Mkurugenzi Mashtaka ili kuona imani ya wananchi  kwa jeshi hilo inaendelea kubakia wakati wote hapa Nchini.
Wito huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizungumza na Kamishna Mpya wa Jeshi la Polisi Zanzibar Kamishna Hamdan Omar Makame aliyefika kujitambulisha rasmi  hapo  katika Ofisi yake iliyopo kwenye jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Balozi Seif  amesema wananchi wamekuwa wakilalamikia matatizo yanayojitokeza kwenye kesi mbali mbali zinazowahusu baadhi ya watu ambazo huleta athari ndani ya jamii  na baadhi yake hufifia bila ya  wahusika kutiwa hatiani kwa madai ya kukosekana kwa ushahidi.
Amesema hali hiyo ikiachiliwa kuendelea ambayo iko chini ya dhamana ya uwajibikaji wa vyombo hivyo viwili inaweza kuleta sura mbaya na matokeo yake itafikia wakati wananchi kujichukulia hatua mikononi mwao.

“ Tumeshuhudia matukio mbali mbali yenye kutia wasi wasi kwa  jamii katika maeneo yao vikiwemo vitendo vya mauaji, udhalilishaji, ujambazi na hata hili lililoibuka la watu kumwagiwa tindi kali. Lakini matokeo yake uchunguzi huo hufifia bila ya jibu muwafaka wanalolipata wananchi “. Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliutaka Uongozi wa Jeshi hilo kuzidisha mashirikano yake na wananchi pamoja na taasisi zote ili kuona  usalama wa raia na mali zao unaendelea kupatikana hapa nchini.
Balozi Seif alimueleza Kamishna huyo mpya wa Polisi Zanzibar kwamba Ofisi yake kwa vile ndiyo inayoratibu masuala yote ya Muungano hapa Zanzibar itakuwa tayari wakati wote  kumpa ushirikiano utakaomuwezesha  kutekeleza vyema jukumu alilokabidhiwa na Taifa  yeye na askari wake.

“ Ofisi yangu ndio iliyopewa jukumu la kuratibu masuala yote yanayohusu mambo ya Muungano kwa hapa Zanzibar. Hivyo nakuhakikishia kwamba mlango wa Ofisi yangu utakuwa  wazi wakati wowote unapopata tatizo la kiutendaji usione tabu kunifuata “. Alisisitiza Balozi Seif.
Hata hivyo Balozi Seif alimueleza Kamishna Hamdan Omar Makame   kwamba  ipo  changa moto hasa wakati wa muelekeo wa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 jambo ambalo jeshi hilo linapaswa kujipanga mapema katika kuhakikisha amani ya jamii inaendelea kuwepo Nchini.
Mapema Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame  alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba atatekeleza vyema majukumu aliyokabidhiwa na Taifa katika misingi ya haki na uadilifu.

Kamishna Hamdan  aliyepewa jukumu la  kusimamia Kamisheni ya Polisi Zanzibar alieleza kwamba anachokitarajia katika  muda wote wa utumishi wake ni kupata ushirikiano wa karibu kutoka pande zote mbili zile za viongozi pamoja na raia wa kawaida.
Kamanda Hamdan Omar Makame  alipandishwa cheo na Jemedari Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwa Kamishna wa Polisi Tarehe 3/12/2013  na baadaye kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Nafasi hiyo ya Ukamishna Zanzibar ilikuwa ikishikiliwa na Bwana Mussa Ali Mussa ambaye kwa sasa ameteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Kamishna wa Polisi Jamii.
View detail

Saturday, August 31, 2013

OFISI YA MKUU WA POLISI YAKUTWA NA KICHWA CHA BINADAMU ALIYEFARIKI

Polisi nchini Kenya
Polisi nchini Kenya wanachunguza kisa ambacho kichwa cha mtu aliyeuawa kilipatikana kimewekwa nje ya afisi ya mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya polisi Johnston Kavuludi jijini Nairobi.
Kifurushi hichi kilichokuwa kimefungwa kwa karatasi ya plastiki, vilevile kilikuwa na mikono miwli ya binadamy iliyojaa damu.
kando ya kifurishi hicho kulikuwa na ilaani iliyoandiskwa ''Kavuludi wewe ndiye utakayefuata''.
Tangu uteuzi wake, kamishna huyo ameongoza harakati za kujaribu kuifanyia marekebisho idara ya polisi ambayo inadaiwa kuwa fisadi zaidi Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa idara ya polisi, hakuna mshukiwa aliyekamatwa kauhusiana na tukio hilo na kuwa bado wangali wanachunguza mwili huo ulikuwa wa nani.
Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na uhasama kati ya tume hiyo inayoongozwa na Kavuludi na ofisi ya mkuu wa polisi, huku zikilumbana kuhusu nani ana madaraka ya kuliendesha idara hiyo.
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop