Saturday, January 26, 2013

MASASI NAKO HAKUKALIKI, VURUGU KUBWA WANANCHI HAWATAKI GESI ITOKE. GARI NA NYUMBA YA MBUNGE NA MAHAKAMA YA MWANZO VYATEKETEA KWA MOTO

 Gari la maji yakuwasha lahisiwa halina maji, askari walipanda wakashuka kulikimbia
Habari nilizozipata hivi punde kutoka Masasi ni kuwa maandamano yameanza tena na safari hii yanaongozwa na dereva boda boda ambao wameingia barabarani.
Risasi za moto na mabomu ya machozi yanapigwa kutawanya watu na tayari nyumba moja imechomwa moto. Gari la maji ya kuwasha limefika ila bado watu wanazidi kuongezeka
Tayari gari na nyumba ya mbunge imechomwa moto na vijanga wanazidi kusonga mbele wakiwa na madumu ya petrol
Mahakama ya mwanzo imechomwa.moto na polisi wamejifungia ndani.wanarusha mabomu ya machozi wakiwa ndani. Askari magereza wamejaribu kuwasha gari la maji ya kuwasha lakini bahati mbaya halina.maji hivyo wakashuka na kukimbia na wananchi wanataka kulichoma moto
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About