Saturday, January 26, 2013

MTWARA HAKUKALIKI! NYUMBA YA HAWA GHASIA YACHOMWA MOTO, MWANDISHI WA CHANEL TEN AJERUHIWA. POLISI WA MTWARA WAZIDIWA. POLISI LINDI NA SONGEA WAENDA KUONGEZA NGUVU. SERIKALI IKO KIMYAA!!


Askari wa kutuliza ghasia wakijiandaa kuzuia vurugu zilizotokea Mtwara, leo kwa kile kilinachodaiwa ni mwendelezo wa vurugu za madai ya gesi.

 

Katika vurugu hizo, mwandishi wa habari wa Chanel Ten, amejeruhiwa kichwani na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu, huku ikielezwa kuwa watu hao wamevamia Nyumba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia, na kuipiga mawe na kuvunjwa vioo na kuchomwa moto.
 
Aidha imeelezwa kua katika harakati hizo pia Mahakama ya Mwanzo imechomwa moto na kusababisha askari kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu hao na kulazimika Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ, kuingilia kati kutuliza ghasia hizo.
 
Quantity : Add to Cart

1 comment:

  1. Eee,Mungu tunakuomba uiponye inchi yetu ya Tanzania. Tupatie amani, utulivu, upendo na mshikamano. Amen

    ReplyDelete

Labels

Blogroll

Labels

About