Welcome to our online store Portal

Template Information

Saturday, May 4, 2013

Ghala la Silaha la Syria lashambulia na Israel



Ndege ya Israel

Serikali ya Syria bado haikusema kitu kuhusu taarifa kutoka wakuu wa Marekani kwamba ndege za Israel zimefanya mashambulio katika ardhi ya Syria, ambako inaarifiwa ghala ya silaha imeshambuliwa.
Huku nyuma kuna taarifa za mauaji zaidi katika miji ya pwani ya Syria kukiwa na tuhuma kuwa raia wengi wamechinjwa na wanajeshi wa serikali na wanamgambo.Wakuu wanasema makombora yalifyatuliwa kutoka ndege za Israel ambazo ziliruka kwenye anga ya Libnan, nchi ya jirani.
Wanaharakati wanaripoti kuwa mauaji ya pili yamefuatia yale ya kwanza katika eneo hilo-hilo la mwambao kaskazini-magharibi mwa Syria.
Wanasema mauaji ya kwanza yalifanywa kwenye kijiji cha al-Beida cha Wasunni, ambacho kilivamiwa na wanajeshi wa serikali siku ya Alkhamisi.
Wanaharakati wamewataja watu 50 ambao wanasema walichinjwa kati yao wakiwemo wanawake na watoto.
Sasa wanaeleza kisa kama hicho kutokea katika mtaa wa Ras an-Naba wa mji wa pwani wa Banias ulio jirani na al-Beida. Wameonesha picha kwenye internet kama ushahidi, lakini hakuna njia ya kuthibitisha ukweli wa picha hizo.
Picha zinaonesha maiti za wanawake na watoto zimelala ndani ya nyumbao zao, miili mengine imekeketwa na mengine imechomwa.
Mamia ya familia zimekimbia Banias kuelekea kusini kwenye mji wa Tartous, lakini wanaharakati wanasema wakimbizi hao wamezuwiliwa kupata hifadhi katika mji huo.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop