Welcome to our online store Portal

Template Information

Saturday, June 22, 2013

AZIZI COMPUTER DOCTOR YATOA HUDUMA YA BURE KUTUMA SMS DUNIA NZIMA KUPITIA BLOG YAKEI

Bofya palipoandikwa SEND SMS kwa rangi nyekundu kutuma sms bure dunia nzima kupitia blog hii, Baada ya kuona watanzania wengi wanaishi kwa chini ya dola 1 kwa siku, AZIZI COMPUTER DOCTOR imeamua kutoa huduma hii bure kwa kila mtanzania na asiye mtanzania kokote duniani atembeleapo blog hii! Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki ABDULAZIZI S. MNYENGEMA mmiliki wa Blog hii kwa kuitumia elimu yake kwa faida ya watanzania wote na mashabiki wa blog hii popote duniani View detail

Wednesday, June 19, 2013

UFADHILI WA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI KWA MWENYEKUPENDA

Bofya palipoandikwa Register kwa kujisajili na kuweza kupata ufadhili kwa kila mwenyekupenda nafasi hii adimu! Imeletwa kwenu kwa ufadhili wa azizi computer doctor

View detail

Tuesday, June 18, 2013

Generali David Sejusa Aamua Kujilipua Hadhaarani

Jenerali Sejusa akiwa mjini London baada ya kufichuka kwa barua yake

Jenerali wa Jeshi aliyesababisha hali ya mshikemshike au sekeseke nchini Uganda wakati maudhui ya barua aliyoiandika yalipofichuka hadharani amezungumza na www.azizicompdoc.blogspot.com kwa mara ya kwanza.
Generali David Sejusa, mmoja wa maafisa wa juu katika jeshi la Uganda alitaka kufanyike uchunguzi wa tuhuma kuwa kuna mpango wa kuwaua maafisa waandamizi wa jeshi na wa serikali wanaopinga kile kilichotajwa kuwa ni mradi wa Muhoozi, mtoto wa Rais Museveni akiandaliwa kumrithi baba yake.
Magazeti mawili na vituo vya Radio vilifungwa kwa karibu siku kumi wakati maafisa usalama walipokuwa wakijaribu kutafuta barua hiyo.
Tangu barua hiyo ilipotolewa hadharani, Jenerali huyo amekuwa kama yuko mafichoni.
Sejusa anasema kuwa yeye ndiye aliyendaika barua hiyo ila hafahamu vipi ilifika mikononi m,wa vyombo vya habari.
Aidha Sejusa amelaani hatua ya serikali kushambulia vyombo vya habari baada ya barua hiyo kufichuliwa akisema kuwa yeye ndiye alikuwa mwandishi wa barua yenyewe na kuwa serikali ingemsubiri arejee Uganda ndiposa iweze kumhoji kuhusu maudhui ya barua hiyo.
Akizungumza na www.azizicompdoc.blogspot.com, Jenerali Sejusa alisema tatizo kubwa na kitu ambacho anakipagia Uganda ni kutaka kuweka muda ambao rais anapaswa kutawala nchio hiyo. Amelaani uongozi wa Rais Yoweri Museveni akisema kuwa katiba ya nchi inapaswa kulindwa kwa njia yoyote labda hata kutumia nguvu dhidi ya wale wanaoikiuka.
Hata hivyo Serikali ya Uganda imepuuzilia mbali madai hayo ya Jenerali David Sejusa. Akizungumza na www.azizicompdoc.blogspot.com, msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo, amesema madai hayo hayana msingi wowote.
Aidha amesema Uganda inatawaliwa kwa misingi ya katiba ya nchi hiyo na ikiwa Jenerali huyo ana malalamiko ya kikazi au kiutawala anaweza kutumia njia ambazo zimewekwa na katiba ya Uganda.
View detail

MGOMO WA WALIMU KENYA WAANZA UPYA

Walimu wa shule za sekondari na taasisi za juu nchini Kenya


Walimu wa shule za sekondari na taasisi za juu nchini Kenya wameanza rasmi mgomo wao wa kitaifa hii leo baada ya kukosa kuafikia mwafaka na serikali kuhusu kutengewa pesa za kuwalipa marupurupu.
Mgomo huu unakuja baada ya kusomwa kwa bajeti ya serikali wiki jana. Walimu hao wanalalamika kuwa serikali imetenga mabilioni ya pesa kwa ununuzi wa vipakatilishi kwa wanafunzi wa darasa la kwanza badala ya kutumia pesa kwa miradi mingine ambayo ni muhimu zaidi katika sekta ya elimu.
Walimu hao wanasema wataendelea na mgomo wao hadi serikali itakapokubali kuwatimizia matakwa yao.
Pamoja na hilo chama cha walimu hao, kimewataka wanchama wake kusalia nyumbani na kutofunza na badala yake kufika katika makao makuu ya chama cha walimu kwa maagizo zaidi kuhusu hatua wakatazochukua.
Walimu hao wanataka wapewe marupuru ya safari zao pamoja na majukumu ya usimamizi wa shule kuwa sawa na yale wanayolipwa wafanyakazi wengine wa umma.
Pia wanataka swala la kupandishwa vyeo kupewa kipaombele.
Dina gahamanyi alitembelea baadhi ya shule kujionea hali ilivyokuwa. View detail

Monday, June 17, 2013

KLABU YA SUNDERLAND YA UINGEREZA YATEMBELEWA NA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE

Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaoandaliwa kua wachezaji mahiri wa mchezo wa mpira wa miguu hapo baadae
Rais Kikwete akipata maelekezo kutoka kwa mwalimu wa watoto hao namna anavyowaandaa na kuwakuza watoto hao ktk mazingira ya kuujua vizuri mchezo wa mpira wa miguu
Rais Kikwete akiwa ktk picha ya pamoja na watoto waliokuzwa ktk kipaji cha mpira wa miguu toka utoto wao mpaka umri wa miaka 12


View detail

Thursday, June 6, 2013

M 2 THE P ATUA DAR KUMZIKA MANGWEA.

Mau Mau Kenya wafidiwa na Uingereza



 Uingereza imekubali kuwalipa fidia na kuwaomba msahama walioteswa wakati wa ukoloni wa Muingereza Kenya

Serikali ya Uingereza inatarajiwa kuomba msamaha pamoja na kuwalipa fidia manusura wa harakati za ukombozi wa Uhuru wa Kenya Mau Mau.
Waliokuwa wanachama wa vuguvugu hilo waliwasilisha kesi mahakamani kwa mateso na dhuluma walizodai kutendewa na uliokuwa utawala wa ukoloni miaka ya 50.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague, anatarajiwa kutangaza kiwango cha pesa ambazo serikali ya Uingereza iko tayari kutoa kama fidia, duru zikisema kuwa huenda ikawa dola milioni 20
Zaidi ya wakenya 5,000, waliteswa baadhi wakinyanyaswa na waliokuwa wakoloni wa Uingereza.
Uingereza ilipigana vita vikali dhidi ya Mau Mau, waliokuwa wanadai ardhi na kuondoka kwa utawala wa kikoloni.
Manusura wa vita hivyo wamekuwa wakiidai Uingereza kuwalipa fidia kwa miaka mingi.
azizicompdoc.blogspot.com ina habari kuwa bwana Hague atawaomba radhi waathiriwa wa vita vya Mau Mau, wakati akitangaza kiwango cha pesa watakazotoa kama fidia kwao.
Serikali ya Uingereza awali ilikuwa imesema kuwa madai yote ya vitedno walivyofanya wakoloni ni juu ya serikali ya Kenya tangu kuipa uhuru mwaka 1963 na kuwa kwa sasa haiwezi kutakiwa kulipa.
Lakini mwaka 2011, mahakama iliamuru kuwa, wanaodai fidia, Paulo Muoka Nzili, Wambuga Wa Nyingi na Jane Muthoni Mara, walikuwa na haki ya kudai fidia kutoka kwa Uingereza .
Mawakili wao wanasema kuwa Nzili alihasiwa , huku Bwana Nyingi akichapwa vibaya wakati Bi Mara akiteswa kimapenzi katika kambi za mateso ambako waliokuwa wanapinga ukoloni walikuwa wakifungwa.
Baada ya uamuzi wa kesi hiyo, ilirejeshwa katika mahakama kuu ili kuamua pesa watakazolipwa na ofisi ya jumuiya ya madola.
Duru zinasema kuwa serikali ilikumbwa na wakati mgumu kupata mashahidi na stakabadhi muhimu kuweza kuelezea ukweli katika kesi hiyo.
Lakini Oktoba mwaka jana, mahakama iliamua kuwa waathiriwa waliowasilisha kesi hiyo mahakamani walikuwa na haki ya kufidiwa kwani walikuwa na kesi nzito dhidi ya serikali ya Uingereza.
Watatu hao walikuwa wamesema kuwa wangekubali wahusika wa kesi kuafikiana nje ya mahakama lakini pia walikuwa wanataka kufuata sheria kwani waliona wangepata haki katika mahakama.
View detail

Wednesday, June 5, 2013

UMATI WA WATU WAJITOKEZA KUMUAGA ALBERT NGWEA.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz akipita mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Albert Mangwea kutoa heshima zake za mwisho. Rais wa Chama cha Wanamuziki Nchini. Mwili wa marhemu Albert Mangwea ukiwa kwenye jeneza tayari kwa watu kutoa heshima za mwisho Umati wa watu wakiwa wamepanga mstari tayari kwa kwenda kuaga huku kikosi cha msalaba mwekundu na polisi kikiwa stand by. Baadhi ya wasanii wa bongo wakiwa kwenye mstari tayari kwa kuaga. ...

Wageni waliofika msibani Morogoro kwa marehemu Mangwea.  Masufuriya ya chakula kwa watu waliokuwepo msibani morogoro.  Wakipanga jambo kutokana na eneo la nyumbani kwao marehemu Mangwea kuwa padogo. ...





 
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop