Tuesday, September 17, 2013

ICC YAPOKEA USHAHIDI KUTOKA KWA SHAHIDI WA KWANZA KTK KESI YA VIONGOZI WA JUU KENYA


Naibu Rais William Ruto alisindikizwa ICC na kikundi cha wabunge wa chama chake
Shahidi wa kwanza kutoka upande wa mashtaka, amefika mbele ya mahakama ya kimataifa ICC kutoa ushahidi dhidi ya naibu Rais wa Kenya William Ruto.
Mahakama inamlinda shahidi huyo kwa kutoonyosha sura yake.
Ruto anakabiliwa na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007-2008
Kesi dhidi ya Ruto na mshtakiwa mwenzake Joshua Arap Sang, ilianza tarehe 10 mwezi Septemba, baada ya wawili hao kutuhumiwa katika kuhusika na ghasia hizo za mwaka 2007.
Kumekuwa na wasiwasi kuhusu mashahidi kujiondoa kwenye kesi hiyo wakihofia usalama wao. Mwishoni mwa wiki, mashahidi wanne walijiondoa katika kesi hiyo baada ya kuelezea wasiwasi kuhusu usalama wao ikiwa watatoa ushahidi mbele ya mahakama hiyo.
Wiki jana mkuu kwenye kesi hiyo, aliakhirisha kesi hiyo kwa sababu mashahidi hawakuwa wamefika kwenye mahakama hiyo kutoa ushahidi wao.
Rais Uhuru Kenyatta, anatarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo mwezi Novemba kwa mashtaka sawa na hayo.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About