Polisi katika eneo la Mtwara
Kusini mwa Tanzania wamewazuilia watu wanaoshukiwa kuhudhuria mafunzo ya
kundi la kigaidi la Al - Shaabab.
Washukiwa walikamatwa Jumatatu katika eneo la
milimani baada ya wananchi waliowaona msituni wakifanya mazoezi ya
kijeshi kutoa habari kwa polisiWashukiwa pia walikuwa na silaha zilizokuwa zimetengezwa kienyeji tu.
Zaidi ya hayo, kamanda huyo wa polisi alisema walipokea taarifa za wananachi wiki moja iliyopita, kuhusu kundi hilo ambalo lilikuwa linapata mafunzo msituni.
Polisi wangali wanawahoji washukiwa hao wakitaka kujua miongoni mwa mambo mengine wadhamini na wafadhili wao.
Kamanda wa polisi alimtaja kiongozi wa kundi hilo kuwa Mohammed Makande mwenye umri wa miaka 39.
Kwa mujibu wa polisi, washukiwa watafikishwa mahakamani mara baada tu ya uchunguzi kukamilika.
Kukamatwa kwao kunakuja wakati ambapo visa vya ugaidi vimeongezeka katika kanda ya Afrika Mashariki hususan nchini Kenya na Somalia.
Wiki jana Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, aliwataka wananchi kuchukua hatua zaidi huku serikali ikidhibiti hali ya usalama katika maeneo yaliyo katika hatari ya kushambuliwa. Tufuatilie kujua nani ni mfadhili mkuu wa kundi hili
zeloth acha unafiki magaidi hawawezi kuwa na panga ,simu na unga kilo 50 tafuteni magaidi hao green guard mnajifanya hamuwaoni mnakwenda kukamata masikini wa watu huo ni unafiki tu
ReplyDelete