Welcome to our online store Portal

Template Information

Tuesday, October 8, 2013

WAMJUA MDHAMINI WA KUNDI LINALODAIWA ALSHABAAB MTWARA?


Polisi walisema walipokea taarifa wiki moja kabla ya kukamatwa kwa washukiwa
Polisi katika eneo la Mtwara Kusini mwa Tanzania wamewazuilia watu wanaoshukiwa kuhudhuria mafunzo ya kundi la kigaidi la Al - Shaabab.
Washukiwa walikamatwa Jumatatu katika eneo la milimani baada ya wananchi waliowaona msituni wakifanya mazoezi ya kijeshi kutoa habari kwa polisi
Kwa mujibu wa kamanda mkuu wa jeshi eneo la Mtwara,Zelothe Stephens, washukiwa hao 11 walikamatwa katika eneo la milimani la Makolionga wakiwa na nyaraka na kanda za video zenye mafunzo ya kundi la Al Shaabab.
Washukiwa pia walikuwa na silaha zilizokuwa zimetengezwa kienyeji tu.
Zaidi ya hayo, kamanda huyo wa polisi alisema walipokea taarifa za wananachi wiki moja iliyopita, kuhusu kundi hilo ambalo lilikuwa linapata mafunzo msituni.
Polisi wangali wanawahoji washukiwa hao wakitaka kujua miongoni mwa mambo mengine wadhamini na wafadhili wao.
Kamanda wa polisi alimtaja kiongozi wa kundi hilo kuwa Mohammed Makande mwenye umri wa miaka 39.
Kwa mujibu wa polisi, washukiwa watafikishwa mahakamani mara baada tu ya uchunguzi kukamilika.
Kukamatwa kwao kunakuja wakati ambapo visa vya ugaidi vimeongezeka katika kanda ya Afrika Mashariki hususan nchini Kenya na Somalia.
Wiki jana Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, aliwataka wananchi kuchukua hatua zaidi huku serikali ikidhibiti hali ya usalama katika maeneo yaliyo katika hatari ya kushambuliwa. Tufuatilie kujua nani ni mfadhili mkuu wa kundi hili

Related Product :

1 comment:

  1. zeloth acha unafiki magaidi hawawezi kuwa na panga ,simu na unga kilo 50 tafuteni magaidi hao green guard mnajifanya hamuwaoni mnakwenda kukamata masikini wa watu huo ni unafiki tu

    ReplyDelete

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop