Mjumbe
wa Halmashauri kuu (NEC) CCM Taifa manispaa ya Singida, Bw. Hassan
Mazala akizindua ofisi mpya ya CCM kitongoji cha Mwachichi kata ya
Mankoko jimbo la Singida mjini.
Na Nathaniel Limu, Mwankoko
MJUMBE
wa Halmashauri kuu CCM (NEC) taifa Manispaa ya Singida, Hassan Mazala
amewahimiza wana CCM kuongeza bidii kukiimarisha chama ikiwemo kujenga
ofisi bora za ngazi mbali mbali kama njia mojawapo ya kukipambanua
chama dhidi ya vyama vya upinzani.
Mazala
ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa ofisi
ya tawi jipya la kijiji cha Mwachichi kata ya Mwankoko, Manispaa ya
Singida.
Amesema
CCM ni chama kikongwe chenye sera zinazotekelezeka, chama kisichokuwa
na sera ya matusi, hivyo ni lazima kionyeshe wazi kwamba hakina chama
cha siasa kinachoweza kufananishwa nacho.
Mazala
amesema wanaccm jukumu lao ni kuhakikisha kila kikicha, CCM izidi
kuimarika kwa kuongeza wanachama na kujenga ofisi bora za ngazi mbali
mbali.
Mjumbe
wa halmashauri kuu (NEC) CCM Taifa manispaa ya Singida, Hassan Mazala
akizungumza na Wana CCM na wakazi wa kijiji cha Mwankoko manispaa ya
Singida muda mfupi baada ya kuzindua ofisi ya CCM kitongoji cha
Mwachichi.
Akifafanua
zaidi, Mnec huyo amesema kuwa ofisi bora zinazofanna na wakati
uliopo,zitasaidia viongozi kuwa na mahali sahihi pa kupanga mipango.
Wanachama pia watapata mahali pa kutolea kero na maoni yao ya
kukiendeleza chama.
“Sasa
kama chama hakina ofisi wanachama wake watajivunia nini watapeleka wapi
kero zao, wataziwasilisha barabarani”, alihoji Mazala na kushangiliwa
kwa nguvu.
Amesema
vyama vya siasa vya upinzani kikiwemo CHADEMA, viendelee tu kutoa
matusi kwenye mikutnao viongozi kufukuzana na kupandikiza chuki na
kupotosha wananchi, wakati huo huo CCM, kitaendelea kujiimarisha.
Baadhi
ya Wana CCM na wakazi wa kata ya Mwankoko,waliohudhuria ufunguzi wa
ofisi mpya ya CCM kitongoji cha Mwachichi uliofanywa na Katibu wa
Halmashauri kuu (NEC) CCM Taifa manispaa ya Singida.
“Katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kila chama kitavuna kilichopanda. Nina
uhakika wananchi watakipambanua Chama Cha Mapinduzi kwa kukipa kura za
kutosha kuliko chama cho chote cha siasa kikiwemo CHADEMA”,amesema.
Wakati
huo huo, Mazala aliwakumbusha viongozi wa ngazi mbali mbali kuongeza
kasi ya kueleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha
uongozi wa serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.
Kikundi
cha uhamasishaji cha CCM kata ya Mwankoko manispaa ya Singida kikitoa
burudani kwenye hafla ya uzinduzi wa ofisi mpya ya CCM kitongoji cha
Machihi.
(Picha na Nathaniel Limu).
0 comments:
Post a Comment