Saturday, November 23, 2013

KIFO CHA DR MVUNGI CHAIBUA MENGI

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,imekamata vielelezo vya mtu anayedaiwa kuiba Kompyuta Mpakato (laptop) ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, marehemu Dk Sengondo Mvungi.
Kamishna wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleiman Kova alitaja vielelezo hivyo kuwa ni pamoja na picha ya mtuhumiwa anayedaiwa kuiba kompyuta hiyo (jina linahifadhiwa).
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, uchunguzi wa kipolisi unaonyesha kuwa, mtuhumiwa huyo ambaye bado hajakamatwa anadaiwa kujihusisha na masuala mbalimbali ya uhalifu jijini Dar es Salaam.
Alisema kompyuta hiyo inadaiwa ilikuwa na taarifa muhimu za kikazi za Dk Mvungi.
“Vielelezo vilikamatwa wakati polisi wakiwa kwenye msako wa kuwatafuta wahusika wa tukio la mauaji ya  Dk Mvungi” alisema.
Kamanda Kova aliwaonyesha waandishi wa habari picha ya mtuhumiwa huyo anayedaiwa bado anaimiliki kompyuta ya Dk Mvungi.
Katika hatua nyingine, Kamanda Kova alisema, polisi inamshikilia mtu aliyedaiwa kujifanya askari,aliyeachishwa kazi mwaka 2003 katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
Askari huyo anadaiwa kukamatwa katika eneo la Mivinjeni akiwa na mtuhumiwa mwingine mkazi wa Kinondoni B, wakiwa katika harakati za kupora gari aina ya Kenta lililokuwa limebeba sigara zenye thamani ya Sh200 milioni.
Kova alisema, uchunguzi umebainika watuhumiwa hao pia ni washiriki kwenye matukio ya  wizi wa fedha kwenye  Benki za Habib na I&M  za Dar es Salaam.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About