Rais Jakaya Mrisho
Kikwete wakati alipokutana na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na
Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath
Pushpakumara (shati jeupe) na ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka,
kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao
likiwamo zao la Mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akipokea zawadi inayotokana na zao la mnazi toka kwa Waziri wa
Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka,
Mheshimiwa Jagath Pushpakumara (shati jeupe) na ujumbe wake mjini
Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na
maradhi ya mazao likiwamo zao la Mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la
mnyauko.
Picha ya pamoja ya
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na
Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath
Pushpakumara (shati jeupe) na ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka,
kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao
likiwamo zao la Mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko. (PICHA
NA IKULU).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amesema kuwa Serikali imedhamiria kukabiliana na maradhi ya mazao
likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
Aidha,
Rais Kikwete amesema kuwa ni muhimu kwa Serikali kuchukua hatua za
kukabiliana na tatizo la minazi kwa sababu watu wengi katika baadhi ya
maeneo ambayo uchumi wake unategemea zao la mnazi wanakabiliwa na hatari
ya kweli kweli ya kuathirika kwa maisha yao.
Rais
Kikwete ametoa uhakikisho huo jana, Jumamosi, Novemba 16, 2013, wakati
alipokutana na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la
Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara na ujumbe wake
mjini Colombo. Waziri huyo aliandamana na Mwenyekiti wa Taasisi ya
Utafiti ya Minazi ya Sri Lanka.
Rais
Kikwete yuko nchini Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) uliomalizika, Jumapili, Novemba
17, 2013. Mkutano huo wa siku tatu, ulianza juzi, Ijumaa, Novemba 15,
2013.
Mheshimiwa
Pushpakumara na ujumbe wake walikuwa wanamwelezea na kumkabidhi Rais
Kikwete Ripoti ya Magonjwa ya Minazi iliyoandaliwa na wataalam wa minazi
wa Sri Lanka ambao walitembelea Tanzania Julai mwaka huu.
Wataalam
hao walitembea Tanzania na kufanya utafiti kuhusu ugonjwa unaolikabili
zao la minazi kufuatia ahadi ya Rais Mahinda Rajapaksa aliyoitoa kwa
Rais Kikwete wakati alipofanya ziara rasmi ya Tanzania Juni 27, 2013, na
baadaye kushiriki katika Mkutano wa Smart Partnership Juni mwaka huu.
Rais
Rajapaksa alitoa ahadi hiyo baada ya kuelezwa na Rais Kikwete kuhusu
zao la kukauka kwa minazi nchini. Minazi ni zao muhimu sana katika
uchumi wa Sri Lanka na ni zao tegemeo kwa wananchi wa Taifa-Kisiwa hilo
kilichoko kusini mashariki mwa India katika Bahari ya Hindi.
Wataalamu
waliofuatana na Waziri huyo wamemwambia Rais Kikwete kuwa ugonjwa
unaolikabili zao hilo la minazi ambao pia unashambulia minazi katika
eneo la Caribbean hauna tiba kwa sababu mpaka sasa hakuna taasisi yoyote
ya utafiti imegundua dawa hiyo.
Wataalam
hao ambao walikaa Tanzania kwa wiki moja, zikiwamo siku mbili katika
Zanzibar, wanasema kuwa zao hilo la mnazi, kama ilivyo katika nchi
nyingine zinazolima zao hilo, lina uwezo mkubwa wa kusaidia uchumi
kupitia viwanda vidogo vidogo.
Wakati
wakiwa Tanzania, wataalam hao wa Sri Lanka walifanya uchunguzi na
utafiti kwa karibu na wataalam wa Taasisi ya Utafiti ya Kilimo ya
Mikocheni (MARI).
0 comments:
Post a Comment