Mwenyekiti
wa Wabunge wa Afrika Mashariki toka Tanzania, Alhaji Adam Kimbisa
akizungumza na waandishi wa habari juu ya hotuba ya Mhe Rais Jakaya
Kikwete na msimamo wa Watanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Kushoto ni katibu wa Wabunge wao, Bi Shy-Rose Bhanji.
Katibu
wa Wabunge wa Afrika Mashariki toka Tanzania Mh. Shy-Rose Bhanji
(kushoto) akizungumzia umuhimu wa Amani katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki na nchi za maziwa makuu, Kulia ni Mwenyekiti wa Wabunge hao
Alhaji Adam Kimbisa.
Katibu
wa Wabunge wa Afrika Mashariki -Tanzania Mh. Shy-Rose Bhanji akionyesha
kitabu cha Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye
ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mwenyekiti wake Alhaji Adam Kimbisa.
WABUNGE
wa Afrika Mashariki toka Tanzania wamesema mkataba wa uanzishwaji wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki ni lazima uwe wa wananchi kwa manufaa ya
wananchi (People Centred Integration) na isiwe ya viongozi. MOblog
inaripoti.
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini
Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki toka Tanzania,
Alhaji Adam Kimbisa amesema wananchi washirikishwe katika kila hatua na
kila ngazi ili waweze kushiriki kikamilifu kwa ajili ya maslahi yao.
“Jambo
la msingi ambalo hata mkataba wa uanzishwaji wa jumuiya imesema wazi
kwamba Jumuiya lazima iwe ni ya wananchi kwa manufaa ya wananchi na
isiwe ya viongozi wa Afrika Mashariki,” amesema Kimbisa.
Amesema
Wabunge wanaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki
wanampongeza Rais Jakaya Kikwete kufuatia hotuba yake aliyoitoa bungeni
mjini Dodoma hivi karibuni na kuelezea masuala kadhaa ya utengamano
baina ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki.
Kimbisa
alisisitiza kuwa Rais alifanya uchambuzi wa kina kuhusu matatizo
yaliyoikumba jumuiya kufuatia mikutano mitatu iliyofanywa na nchi tatu
za Kenya, Uganda na Rwanda ikiwatenga Tanzania na Burundi.
Amesema
vile vile kuweka wazi msimamo sahihi wa Tanzania kuendelea kuwepo
katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba Tanzania haitajitoa.
Kwa
Upande Katibu wa Wabunge wao wa Afrika Mashariki, Bi Shy-Rose Bhanji
amesema kama wabunge wanampongeza Mhe Rais Kama Amiri Jeshi Mkuu wa
Kupeleka kikosi kimoja cha wanajeshi katika Brigedi Maalum iliyoundwa na
Umoja wa Mataifa ili kuongeza nguvu ya udhibiti wa waasi Mashariki ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
“sisi
tunaamini amani ni jambo la msingi katika Afrika Mashariki na hasa
katika nchi zilizo katika maziwa makuu, tunawapongeza wanajeshi wetu na
wanajeshi maalum wa umoja wa mataifa kwa kazi nzuri walioifanya,”
“Tunaamini
kwamba suluhisho la matatizo ya nchi za maziwa makuu yatapata ufumbuzi
wa kudumu iwapo kutakuwa na utaratibu wa kukaa meza moja kwa pande zote
husika na kufanya mazungumzo ya kuleta Amani,” amesema Bhanji.
0 comments:
Post a Comment