Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP. Geofrey Kamwela akitoa taarifa
kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya matukio ya kuuawa
watu wawili mkoani Singida, likiwemo la Egila Petro kumpiga kwa fimbo
mama mkwe wake mwenye umri wa miaka 80 na kusababisha kifo chake. Mmoja ampiga fimbo kichwani mkwewe, kisa amechoka kumlea
Watu
wawili mkoani Singida wamefariki dunia kwenye matukio tofauti likiwemo
la kikongwe mmoja mwenye umri wa miaka 80, kupigwa fimbo kichwani na
mkwewe kwa kile kilichodaiwa kuwa mkwewe huyo, amechoka kumlea.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida SACP,Geofrey Kamwela, amesema Egila Petro
(42) mkazi wa kijiji cha Mpora kata ya Iseke tarafa ya Nkoko wilayani
Manyoni amempiga fimbo kichwani mama mkwe wake Doris Chiwiche na
kumsababishia kifo chake siku tisa baadaye.
Amesema
kikongwe huyo Doris alipigwa fimbo kichwani na Egila Novemba 18 mwaka
huu saa nane mchana na alifariki Novemba 27 mwaka huu saa 12 asubuhi.
Kamwela
amesema chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa chini kwa chini kati ya
Egila na mama mkwe wake Doris huku ikidaiwa kuwa Egila amekuwa
akimshinikiza mumewe Benard Mdemu amwondoe mama yake huyo na kumpeleka
kwa ndugu zake wengine kwa vile yeye amechoka kumlea.
Katika
tukio jingine Kamanda Kamwela amesema John Liongo (37) mkazi wa Misuna
Singida mjini amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kichwani na
tumboni na watu wasiojulikana.
Amesema
tukio hilo limetokea Novemba 27 mwaka huu saa 6.10 mchana huko katika
kijiji cha Mnang’ana kata na tarafa ya Sepuka wilayani Ikungi.
“Uchunguzi
wa awali unaonyesha kuwa marehemu akiwa na watu wasiojulikana siku ya
tukio aliondoka Singida mjini kwa gari ambalo bado halijajulikana namba
zake za usajili Walipofika katika kijiji cha Mnang’ana waliingia porini
na huko ndiko walipomuulia John”,alifafanua Kamwela.
Kamanda
huyo amesema katika eneo hilo la mauaji waliokota maganda watatu ya SAR
na SMG ambayo risasi zake zilitumika kumuulia John.
“Niseme
tu kwamba uchunguzi zaidi bado unaendelea kwa lengo la kuwabaini wauaji
hao waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria”,amesema.
0 comments:
Post a Comment