Askofu
Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha Josephat Lobullu (kulia) na
Askofu wa Jimbo la Same Rogath Kimaryo wakiongoza ibada ya mazishi ya
aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi.
Ibada hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chanjale wilayani Mwanga mkoani
Kilimanjaro na kuhudhuriwa pia na Askofu Damian Dallu (katikati) wa
Jimbo la Geita Jumatatu, Novemba 18, 2013.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, mkewe Mama Tunu, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba Jaji Joseph Warioba na viongozi wengine wakifuatilia ibada ya
mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt.
Sengondo Mvungi. Mazishi hayo yalifanyika kijijini Chanjale wilaya ya
Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba 18, 2013.
Familia
ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo
Mvungi ikifuatilia ibada ya mazishi iliyofanyika katika kijijini
cha Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18,
2013.
Jeneza
lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt.
Sengondo Mvungi likishushwa kaburini wakati wa mazishi yaliyofanyika
kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba
18, 2013.
Askofu
Damian Dallu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita akiongoza ibada ya
mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu
Dkt. Sengondo Mvungi katika makaburi ya familia kijijini Chanjale wilaya
ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
Mke
wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu Dkt.
Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi akiweka shada la maua katika kaburi la
mume wake wakati wa mazishi kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani
Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
Waziri
wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James
Mbatia wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi wakati wa mazishi kijijini
Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18,
2013.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda jana (Jumatatu, Novemba 18, 2013) aliongoza mamia ya
waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume na Mabadiliko
ya Katiba na Kiongozi wa NCCR-Mageuzi Dkt. Sengomdo Mvungi yaliyofanyika
katika kijiji cha Chanjale wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Pamoja
na Waziri Mkuu aliyeongozana na mkewe, Mama Tunu, pia walikuwepo
Mawaziri kadhaa kiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uratibu na
Uhusiano) Steven Wassira aliyekabidhi ubani wa Rasi Jakaya Kikwete kwa
familia.
Ibada
ya mazishi iliendeshwa na Maaskofu watatu wakiongozwa Askofu Mkuu wa
Jimbo la Kanisa Katoliki Arusha, Josephat Lebullu ambaye ni mwenyeji wa
wilaya ya Mwanga. Wengine walikuwa Askofu wa Jimbo la Same Rogath
Kimaryo na Askofu wa Jimbo la Geita Damian Dallu aliyesafiri kutoka
Geita kuja kuungana na wenzake kumuaga Dkt. Mvungi.
Pamoja
na Waziri Mkuu, mazishi hayo pia yalihudhuriwa na zaidi ya nusu ya
wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti wake
Jaji Joseph Warioba. Mawaziri wengine waliokuwepo ni Prof. Jumanne
Maghembe (Maji) ambaye pia ni Mbunge wa Mwanga.
Wengine
ni Dkt. Harrison Mwakyembe (Uchukuzi) na Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria Angellah-Jasmine Kairuki. Pia walikuwepo Wakuu wa mikoa ya Arusha
(Mugessa Mwalongo) na Kilimanjaro Leonidas Gama.
Kwa
upande wa NCCR-Mageuzi, uongozi wote wa juu wa Chama hicho ulikuwepo
ukiongozwa na Mwenyekiti wake James Mbatia ambaye aliiomba Serikali
kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.
Pamoja
nao, kulikuwa na wawakilishi kadhaa wa taasisi mbalimbali ambazo
marehemu Dkt. Mvungi alifanya nazo kazi wakati wa uhai wake. Taasisi
hizi ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambacho kiliwakilishwa na
Mkuu wa Shule Kuu ya Sheria Prof. Bonaventure Rutinwa, Kituo cha Sheria
na Haki za Binadamu (LHRC) kilichowakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji
Dkt. Hellen Kijo-Bisimba; Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) na Chama cha
Wanasheria Tanzania Bara (TLS) kilichowakilishwa na Wakili Eric Ngimaryo
na mawakili wengine kadhaa kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
Dkt.
Mvungi alifariki nchini Afrika Kusini alikokuwa amepelekwa kwa ajili ya
uchunguzi na matibabu Zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI)
alikokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani
usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.
0 comments:
Post a Comment