Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk
Wilbrod Slaa amepokewa kwa mabango katika mkutano wake wa hadhara
wilayani Kakonko, Kigoma lakini akawaambia waliofanya hivyo kuwa chama
chake hakitayumbishwa huku akiwataka wanaosimama na mabango kumtetea
Zitto Kabwe kung’oka naye ndani ya chama.
Dk Slaa yuko mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya
ziara yake ya siku 11 kutembelea Mikoa ya Shinyanga na Kigoma kukagua na
kuimarisha uhai wa chama.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye Uwanja wa Mwenge Kakonko, Dk Slaa alisema Chadema ni chama imara
na kinaendeshwa kwa misingi ya katiba na kanuni.
“Hakuna kiongozi aliye juu ya katiba, ninawaasa wote wanaobeba mabango kujiangalia kwa kuwa ninafahamu wanatumiwa.”
Kabla ya kupokewa kwa mabango hayo, Dk Slaa
aliyewasili Kakonko saa 5:11 asubuhi akitokea Wilaya ya Kahama,
Shinyanga alikwenda moja kwa moja katika Kata ya Mhange ambako alifanya
mkutano wa hadhara.
Dk Slaa alikumbana na mabango hayo saa 8:45 mchana msafara wake ulipowasili Kakonko Mjini ukitokea Mhange.
Wakati Dk Slaa akiingia katika uwanja wa mkutano,
ulio jirani na Ofisi za CCM Wilaya ya Kakonko, kuliibuka kundi la vijana
wapatao watano wakiwa na mabango mkononi na kuanza kukimbia kuyafuata
magari matatu ya msafara wa Dk Slaa huku wakionyesha mabango yao. Hatua
hiyo iliwafanya polisi waliokuwapo eneo hilo la mkutano kuwazuia na
kuanza kuwatimua lakini mara baada ya Dk Slaa kuteremka katika gari yake
na kuingia uwanjani hapo, aliomba kipaza sauti na kuwataka askari hao
kuacha kuwatimua wenye mabango. “Naomba msiwaondoe waacheni waje...
waruhusuni kwenye mkutano na mabango yao. Waacheni waje hapa …
msiwazuie, waacheni waonyeshe mabango yao na muwaruhusu tu wapite hapa
mbele, msiwapige tafadhali,” alisema Dk Slaa.
Baada ya kauli hiyo, polisi waliwaruhusu vijana
hao watano ambao walibakiwa na mabango manne, moja likiwa limechanika
walipokuwa wanawazuia.
Mabango hayo yaliyokuwa na maandishi ya aina moja,
yalikuwa na ujumbe uliosomeka: “Tanzania Kigoma Kakonko bila Zitto
Haiwezekani”, ‘Mhe. Slaa, Mhe. Mbowe mnatakiwa kujiuzuru mara moja” na
jingine lilisomeka; “Hatupo tayari kwa kusikiliza lolote bila ya Zitto”.
Mara baada ya kupanda jukwaani Dk Slaa aliwataka
tena wenye mabango kusogea karibu na jukwaa kuu alipokuwa amesimama na
kuanza kuwauliza maswali vijana hao iwapo wanajua Katiba ya Chadema na
kama wana kadi za chama. “Naomba niwaulize, hivi nyie wenye mabango
mnaijua Katiba ya Chadema?” Walimjibu: “Hapana.” Dk Slaa akawauliza
tena: “Sasa mnadai nini kwa mabango yenu kama hamjui Katiba ya Chadema?”
Mmoja wa walioshika mabango hayo alijibu: “Mtetezi wetu Zitto.”
Kutokana na hali hiyo Dk Slaa aliwauliza, atakuwa
amekosea akiwakabidhi kwa Polisi kuwa siyo wanachama wa Chadema lakini
wanafanya vurugu katika mkutano halali?
Kabla ya kutoa majibu, baadhi ya wanachama na mashabiki wa
Chadema walimbaini kuwa mmoja wa waliobeba mabango hayo anafahamika na
ni mtoto wa mmoja wa viongozi wa CCM, hatua ambayo iliwafanya watu
waliokuwa wakisikiliza kuanza kumzomea na vijana hao kuinuka na kuanza
kuondoka huku wakiendelea kuzomewa.
Baada vijana hao kuondoka, Dk Slaa aliendelea na
mkutano huku akiwaeleza wanachama wake kuwa kama wanafikiri kufanya
hivyo kunamsaidia aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe
wanakosea.
Dk Slaa alimnanga Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana kuhusiana na kilio chake cha mawaziri mizigo akisema hakupaswa
kulalamikia majukwaani, bali alitakiwa kumshauri Rais Jakaya Kikwete
kuwatimua mara moja.
“Kinana kulalamika jukwaani haisaidii, hii
inaonyesha udhaifu wa CCM ambayo Serikali ndiyo inayotekeleza ilani
yake,” alisema Dk Slaa. Dk Slaa alisema pia kuwa Chadema kitatumia
wabunge wake kuibana Serikali kuhusu fedha za ruzuku ya kilimo
zinazotolewa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo lakini zimekuwa
zikitafunwa na wajanja wachache.
Mpasuko wa kisiasa ndani ya Chadema katika Tawi la
Mwandiga, Jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma ulioibuka baada ya
Kamati Kuu ya chama hicho kumvua madaraka Zitto ambaye pia ni mbunge wa
jimbo hilo, haujapata suluhu.
Wakati hali ikiwa hivyo, kuna taarifa za chini kwa
chini kuwa baadhi ya viongozi wamekwepa kuungana na Dk Slaa katika
ziara hiyo.
Hata hivyo, ilielezwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema
Mkoa, Jafari Kasisiko hayumo kwenye msafara huo kwa kuwa ni mgonjwa
wakati Katibu wa Mkoa, Msafiri Wamalwa yupo mkoani Tabora kwa shughuli
za kifamilia.
Mwenyekiti wa Jimbo la Kigoma Kaskazini (Chadema),
Ally Kisala alisema uongozi wa jimbo hilo unaendelea na mikakati ya
kumpokea Dk Slaa anayetarajiwa kufanya mikutano jimboni humo Desemba 10,
mwaka huu.
Kisala alisema uongozi wa Chadema ulipendekeza
mkutano huo ufanyike katika Kijiji cha Nyarubanda lakini chama ngazi ya
taifa kimeagiza ufanyike Mwandiga, kijiji ambacho kinaonyesha upinzani
dhidi ya ziara hiyo.
Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limesema limeandaa
ulinzi wa kutosha kuhakikisha usalama katika kipindi chote cha ziara ya
Katibu Mkuu huyo wa Chadema.
Kikao kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wa Chadema Tawi la
Mwandiga, Kudra Maulid kwa lengo la kuondoa tofauti zilizojitokeza
miongoni mwa wanachama, kilishindwa kupata suluhu baada ya kila upande
kuushutumu mwingine kuhusika na mpasuko ndani ya chama.
Mvutano ndani ya tawi hilo uliibuka Novemba 24,
mwaka huu, siku mbili tu baada ya Kamati Kuu kumvua Zitto nyadhifa zake
pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo na Mwenyekiti wa
Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Hatua hiyo iliwakera baadhi ya wanachama na wapenzi wa Chadema katika tawi hilo ambao waliandamana na kufanya ghasia.
Katika kikao cha juzi, wanachama walijadili hatima
ya mgogoro huo na madhara yanayoweza kutokea kwa maslahi ya chama na
hivyo kufikia uamuzi wa kuzika tofauti zao licha ya kila upande
kushikilia kwamba upo sahihi.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa wanachama hao walikubaliana kuimarisha chama bila kujali kwamba Zitto ni mzaliwa wa kijiji hicho.
Chama kinachokufa ni ccm.Hebu tazama kwa umakini utaona ccm inatumia nguvu kubwa kupambana na chadema na utaona nguvu yao ccm imegonga mwamba wakina chadema wameshituka mapema na kuwafyeka wasaliti ambao wangekiangamiza chama. ukitazama pia kwa umakini hiliswala utaona limewaogopesha sana ccm. chadema itavuka hiki kikwazo na itachukua dola 2015 kirahisi ccm hawajui wanaipigia debe chadema ishinde kwa vitendo vyao vinavyo onekana waziwazi kama vile kuandaa watu kwa garama kuharibu mikutano ya chadema huko kigoma,kuwanunua wakina zito,kitila, said arfi na wengine wengi nasema wengi kwa sababu pesa aliyopewa zito aliitumia kuwannua viongozi wandamizi wa chadema mikoani. mfano juzi hivi nikiwa ndani sa usafiri mjadala ukaanza 99% wakaunga mkono maamuzi ya kamati kuu chadema mmoja alikuwa akipinga sana basi lote lilimshambulia sana akapigwa swali kwa jinsi alivyokuwa amepaniki akalopoka msaada aliopatiwa na zito mil12 + ushauri wa kibiashara na akajitambulisha yeye ni diwani wa kahama(nyasubi). Hapa ccm wanajichanganya tu watanzania 99% tunaona na tutawapiga chini vibaya kwa aibu!!!
ReplyDeleteChama kinachokufa ni ccm.Hebu tazama kwa umakini utaona ccm inatumia nguvu kubwa kupambana na chadema na utaona nguvu yao ccm imegonga mwamba wakina chadema wameshituka mapema na kuwafyeka wasaliti ambao wangekiangamiza chama. ukitazama pia kwa umakini hiliswala utaona limewaogopesha sana ccm. chadema itavuka hiki kikwazo na itachukua dola 2015 kirahisi ccm hawajui wanaipigia debe chadema ishinde kwa vitendo vyao vinavyo onekana waziwazi kama vile kuandaa watu kwa garama kuharibu mikutano ya chadema huko kigoma,kuwanunua wakina zito,kitila, said arfi na wengine wengi nasema wengi kwa sababu pesa aliyopewa zito aliitumia kuwannua viongozi wandamizi wa chadema mikoani. mfano juzi hivi nikiwa ndani sa usafiri mjadala ukaanza 99% wakaunga mkono maamuzi ya kamati kuu chadema mmoja alikuwa akipinga sana basi lote lilimshambulia sana akapigwa swali kwa jinsi alivyokuwa amepaniki akalopoka msaada aliopatiwa na zito mil12 + ushauri wa kibiashara na akajitambulisha yeye ni diwani wa kahama(nyasubi). Hapa ccm wanajichanganya tu watanzania 99% tunaona na tutawapiga chini vibaya kwa aibu!!!
ReplyDelete