Akiwasilisha mapendekezo hayo jana, Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Profesa Costa Mahalu alisema wanataka Jaji Warioba afanye
kazi moja ya kusoma Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya bungeni.
Profesa Mahalu alisema baada ya hapo wajumbe wa
Bunge Maalumu la Katiba watakuwa na kazi ya kujadili kwa kina Rasimu ya
Katiba kabla ya kuipitisha au kuikataa.
Pendekezo kuhusu Jaji Warioba kusoma Rasimu
bungeni imo katika Kanuni ya Pili ya kanuni ndogo ya (d) ya Rasimu ya
Kanuni, ambayo inampa nafasi Jaji Warioba kuwasilisha kazi aliyoifanya
na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
0 comments:
Post a Comment