Mgombea
ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (32), akiwapungia
wananchi huku akiwa amebebwa alipowasili kwenye mkutano wa kampeni
katika Kijiji cha Mangalali, Kata ya Ulanda, Iringa Vijijini leo
mchana.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akiongoza msafara wa mgombea ubunge
wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa aliyebebwa walipowasili kwenye
mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Mangalali.
Mgimwa
akiungana na wanakijiji kucheza ngoma ya asili ya kabila la Wahehe
alipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe, Kata ya
Ulanda mchana leo.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM, Nchemba (kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa,
Joyce Msamba tavangu (katikati) na mgombea ubunge kupitia CCM, Mgimwa
wakicheza walipofika kwenye kampeni katika Kijiji cha Kibebe.PICHA ZOTE
NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Vijana wakimkaribisha kwa kucheza kijana mwenzao Godfrey Mgimwa katika mkutano huo wa kampeni
Nani zaidi?
Mama
mkazi wa Kijiji cha Kibebe, Venanzila Kihaga akiwa ameshika kipeperushi
cha Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa, alipoteuliwa na
wanakijiji kumuombea kimila Mgimwa ashinde uchaguzi huo utakaofanyika
Machi 16, mwaka huu.
Mchungaji
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Kalenga
Tosamaganga,Kisabugo Mkemwa akitoa mahubiri ya kumuombea Mgimwa
(kushoto) ili ashinde uchaguzi huo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa
CCM, Nchemba.
Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Iringa, Aloyce Mgongolwa akisikiliza
kwa makini wakati Nchemba akihutubia katika mkutano huo wa kampeni
katika Kijiji cha Kibebe.
Balozi wa CCM Tawi la Kibebebe, Julius Kihaga akiwa makini kusikiliza hotuba ya Mgimwa
Ofisa
Mwandamizi wa Mawasiliano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Gabriel
Athuman akinywa maji ya kisima ambayo aliyasifia kuwa ni matamu wakati
wa mkutano wa Kampeni za CCM Jimbo la Kalenga katika Kijiji cha Kibebe
Akina mama wakisikiliza kwa makini wakati Mgimwa akijinaji katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe leo mchana.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, Mgimwa.
Aliyewahi
kuwa Mgombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki kupitia Chadema, na Ofisa
wa Chadema Makao Makuu, Mwampamba akielezea jinsi alivyoamua kujiondoa
kwenye chama hicho baada ya kufanyiwa mabaya na uongozi wa Chadema
ambacho alidai hakifai wananchi kujiunga
0 comments:
Post a Comment