Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao,
wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo juni
23, 2014 akiongozana na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo. Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita. (Picha na OMR).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao,
wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni
23, 2014 akiongozana na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo. Li
Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita. Wa pili (Kulia) ni Balozi
wa Tanzania, nchini China, Luteni General Abraham Shimbo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China,
Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es
Salaam, leo June 23, 2014. Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku
sita.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
(wa pili kulia) na baadhi ya Mawaziri wake, akiwa katika mazungumzo na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, aliyeongozana
na ujumbe wake wakati alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni
23, 2014 kwa ajili ya mazungumzo. Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya
siku sita.
Baadhi ya Mawaziri waliofika katika mazungumzo hayo Ikulu jijini Dar es Salaam, na baadhi kusaini mikataba na watu wa China.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (kulia)
akisainiana mkataba na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa
China, Li Jinzao, wa Makabidhiano ya gari la matangazo la Shirika la
Utangazaji la TBC, yaliyofanyika mapema mwaka huu. Shughuli hiyo ya
kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es
Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, (kulia) akisainiana
mikataba miwili na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China,
Li Jinzao, ya makubaliano ya ushirikiano wa Kitaalamu utakaoiwezesha
China kuwapa mafunzo Wanariadha wa Tanzania nchini China na wa
makubaliano ya awamu ya tatu ya Ushirikiano wa kiufundi baada ya China
kusaidia na kukamilisha Ujenzi wa Uwanja wa Taifa. Shughuli hiyo ya
kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es
Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao.
0 comments:
Post a Comment