Jeshi la Polisi nchini limetangaza kuanzishwa kwa operesheni maalumu ya kuwasaka wasanii wa ngoma wanaocheza wakiwa uchi maarufu kama kigodoro na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Pia, litafanya operesheni ya kuwasaka madereva wa
bodaboda, bajaji na baiskeli za matairi matatu wasiofuata sheria za
usalama barabarani.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senso
alisema “Tunalaani vikali vikundi vya ngoma ambavyo hivi karibuni
vimeibuka kwa wingi na huwa vinafunga mitaa na barabara huku wanawake
wakicheza wakiwa uchi.’’
Hivi karibuni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipiga marufuku ngoma za aina hiyo.
Alisema kuwepo kwa vikundi hivyo ni uvunjaji wa
sheria na maadili ya nchi, jeshi hilo litawasaka popote walipo ili
kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Alisema vikundi vya ngoma vinatakiwa kufuata
utaratibu unaowekwa na halmashauri za maeneo husika ili kuzuia mianya ya
kukiuka maadili.
Akizungumzia tukio la juzi la wachezaji wa
kigodoro kudai kupigwa risasi eneo la Mwananyamala, alisema hakuna
msanii aliyepigwa risasi, waliumia wakati wa purukushani zilizotokea
polisi walipokuwa wakiwatawanya watazamaji wa ngoma hiyo.
“Hata ripoti ya daktari kutoka Hospitali ya
Mwananyamala inaonyesha wacheza ngoma hao hawakupigwa risasi kama
wanavyodai wao,” alisema Senso.
Akizungumzia operesheni ya bodaboda alisema,
“Imekuwa kawaida kwa madereva wa vyombo hivyo kupita barabarani wakati
taa nyekundu zikiwa zinawaka hali ambayo husababisha ajali nyingi.
kutokea.”
Alisema kuanzia Januari mpaka Juni, mwaka huu,
ajali 1,449 zilizosababishwa na vyombo hivyo zilitokea na kusababisha
vifo 218 huku watu 1,304 wakijeruhiwa.
0 comments:
Post a Comment