Friday, June 2, 2017
Monday, September 28, 2015
SAMSUNG POWER BANK YA POWER 20000mAh KWA TSH 60,000
Labels:
power bank
Thursday, September 18, 2014
IUFRO2014 Blog Competition
How to Enter and Win
- Write a blog article that introduces your research or project and how it relates to the overall Congress theme “Sustaining Forests, Sustaining People – The Role of Research”. See the FAQ’s for what makes a good blog post.
- Submit your blog posting with a maximum word count of 750 along with any photos to blog@iufro.org in a .doc or .docx file with the subject line “IUFRO2014 Blog Competition”.
- Ensure to include a caption and credit for any photos submitted.
- Entries must be received by 30th September 2014 (23:59hrs +12 GMT).
- To increase your chances of winning, post your story on Twitter with the hashtags #IUFRO2014 and #RoleOfResearch, and encourage friends to comment, “like” and “share” your post on Facebook, and retweet your post on Twitter. The more views, comments, and votes your article receives the greater your chance of winning.
- The winner who has the most popular article submitted to the #IUFRO2014 Blog Competition will receive a cash prize in the sum of USD 500.
- Two additional finalists will be selected according to the article they submitted based on a popularity ranking with the most page views, comments and highest votes. These persons will receive a copy of “Forests and Globalization: Challenges and Opportunities for Sustainable Development“.
Labels:
Blog Competition
Saturday, September 13, 2014
Tuesday, August 26, 2014
FURSA YA KUSOMESHWA NA MFUKO WA MWL NYERERE KWA WATANZANIA TUU
With effect from the 2013/14 academic
year, the M
walimu Julius K. Nyerere Memorial Scholarship
Fund began granting Scholarship in the United Republic of Tanzania. The Fund
grants scholarship to top best undergraduate female Tanzanian students to pursue
Mathematics and Science studies in Tanzanian universities.
It is also partly used to sponsor
both male and female Tanzanians
top best students to pursue undergraduate
studies in Economics Information Technology, Accounting and Finance as well as best
students intending to pursue Master’s
programmes in those fields
Follow the link for more information
View detail
Follow the link for more information
Labels:
Scholarship
UMESHAWAHI KUJIULIZA KUHUSU KUPATA MAFANIKIO? MAJIBU ULIYAPATA?
Ulishawahi kujiuliza siku moja kua kwanini watanzania wengi tuna uwezo wa kifikra lakini hatufiki popote kwa mawazo na fikra zetu? Je ulishapata jibu? sasa fuatana mimi kujua jibu la swali hili, ni kutokana na kutofikiria tunaanzaje kutekeleza tunalolifikiria ktk vichwa vyetu, tunaipaje nafasi fikra yetu? tunalipaje nafasi wazo letu? je tunaweza kulielezea wazo letu? lakini haya yote niliyapata majibu ktk mafunzo mafupi niliyohudhuria KINUvation ktk mafunzo yalipewa jina la
Design for Development Bootcamp! ambayo yalinifanya nipanue uwezo wangu wa kiakili, kifikra na kuweza kuyawasilisha yale ninayoyafikiri ili yaweze kunisaidia mimi na watu wanaonizunguka bila kumsahau muajiri wangu kunafaika na elimu niliyoipata. Hakika ni pongezi kwao waliofikiria kutuletea mafunzo kama haya KINUvation chini ya usimamizi mkubwa wa Catherinerose Barretto na Mr Max Krueger pongezi kubwa kwa watu hawa
Hakika mafanikio hufurahisha sana pale unapoona ulilofikiri linafanikiwa |
Akili hutulia sana pale unapojiandaa kuonyesha ulilolifikiria na kulifanikisha |
Ni furaha isiyokifani pale ulilionyesha kwa wenzio linafanikiwa |
Hakika maelekezo na mafunzo lazima yafuatwe kabla ya lolote kufanyika |
Inafurahisha kila mtu anapopewa nafasi ya kusikilizwa na kuelezea analolifikiri lingefaa kunufaisha wengine |
Hakika akili ukiituma yaweza kukupa majibu sahihi |
Kila mmoja akipewa nafasi kwa wakati wake maendeleo yanaweza kua makubwa zaidi |
Je na wewe umeshafikiria kuutoa ujuzi ulionao kwa wengine tena bila ya malipo? |
Hakika kila aliye na ujuzi wa jambo anapenda na mwingine aupate ujuzi huo, ni suala la furaha |
Ukiona Fursa huna budi kuifuata na kunufaika nayo |
View detail
Labels:
Mafunzo
Thursday, August 21, 2014
MWINYI ATEMA CHECHE ZAWAGUSA VIONGOZI WAKUBWA NCHINI
Mstaafu
wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifungua semina
ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na
wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa
Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amesema bado viongozi
wa umma wanatumia madaraka yao na Ofisi zao kwa kujinufaisha wenyewe na
kuwasahau wananchi waliowaweka madarakani hivyo kuna kila sababu ya
kuleta sheria ya kuziba mianya hiyo kwa viongozi wanaokwenda kinyume na
maadili.
Alhaj
Mwinyi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua
semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti
Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Alisema
licha ya kuwepo kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995
inayotumika sasa bado kumekuwa na wimbi kubwa la mienendo ya matumizi
mabaya ya ofisi na madaraka kwa viongozi wa umma kwa kujinufaisha
wenyewe kimaslahi.
“…Maana
yake ni kwamba umma sasa haupewi kipaumbele unavyo stahiki. Maamuzi ya
viongozi yanatolewa kwa maslahi binafsi na hivyo kudhihirisha kuwepo kwa
tatizo la mgongano wa maslahi. Viongozi hao waliopewa dhamana na
wananchi wanatumia rasilimali za umma ili kujinufaisha binafsi au
shughuli zao ambazo wanazo pembeni,” alisema Rais huyo mstaafu.
Alisema
hata hivyo sheria ya maadili ya viongozi wa umma imekuwa na mapungufu
kwa kuwabana baadhi ya viongozi wa umma na kuwaacha wengine pamoja na
watumishi wa umma hivyo kujikuta nao wakijihusisha na mgongano wa
kimaslahi.
Hata
hivyo, ameongeza kuwa tayari Serikali imeona mianya hiyo na hivyo
kuanza mchakato wa kuja na sheria maalum itakayo dhibiti hali hiyo.
“…Nadhani mmewahi kusikia mara kwa mara namna ambavyo Rais wetu
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagiza Serikali kufanya jitihada za
dhati ili kuhakikisha kuwa viongozi wa umma wanaacha au wanajiepusha na
tabia ya kushiriki zaidi kwenye biashara na kuacha jukumu lao…,”
alifafanua Mwinyi akiwaeleza washiriki wa semina hiyo.
Aidha
aliipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kuanza
mchakato wa kutungwa kwa sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi
kwa Viongozi wa umma, ambapo itakapo kamilika huenda ikawa suluhisho la
mgongano wa kimaslahi kwa viongozi na watumishi wa umma.
Rais
huyo mstaafu aliwataka wanasemina kuijadili rasimu iliyowasilishwa na
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kutoa maoni yao
kuiboresha zaidi ili itoke na majibu ya kero ya muda mrefu ya Mgongano
wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Kwa
upande wake, Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki, Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus akiwasilisha mada juu ya
Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa
umma kwa wanasemina kabla ya mjadala alisema wataalam wa Sekretarieti
hiyo wamefanya utafiti kwenye mataifa mbalimbali na kutoka na
mapendekezo ambayo yataongoza mjadala kuelekea kupata sheria nzuri.
Naye
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome
Suzete Kaganda akizungumza katika semina hiyo, alisema Rasimu ya Sheria
Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma walioiandaa
itajadiliwa na wadau mbalimbali ili kupata maoni kabla ya kuwasilishwa
kwenye baraza la makatibu wakuu kuboreshwa zaidi kabla ya mchakato
kupanda ngazi za juu.
Aidha
aliwataka wananchi na wadau wengine kuendelea kuijadili Rasimu ya
Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma pindi
itakapo wafikia na kutoa maoni kwa lengo la kuiboresha zaidi ili itakapo
kamilika iweze kufanya kazi vizuri na kujibu kero zilizopo katika eneo
hilo la viongozi wa umma.
“…Mapendekezo
ya sheria hii hayalengi kuwafanya viongozi kuwa maskini, bali kasi yao
ya ukwasi iendane na hali halisi ya kipato chao. Sheria hii
itakapopitishwa itapunguza ubinafsi wa viongozi walioko madarakani
kujipendelea wenyewe na maeneo wanayotoka.” Alifafanua Jaji Kaganda.
View detail
Labels:
Rais mwinyi
Design for Development Bootcamp
Interested in creating technologies and enterprises
that improve the lives of people living in poverty? In this full day
hands on workshop you will be introduced to the design cycle and and
collaboratively work on solutions to real world problems
The workshop is co-hosted by Kinu and alumnus of this years International Development Design Summit (IDDS) in Arusha, who will introduce you to some of the concepts and tools used at IDDS.
Follow the link for more Information View detail
The workshop is co-hosted by Kinu and alumnus of this years International Development Design Summit (IDDS) in Arusha, who will introduce you to some of the concepts and tools used at IDDS.
Follow the link for more Information View detail
Labels:
Hosted by KINUvation
Wednesday, August 20, 2014
WANAFUNZI WA STASHAHADA YA UALIMU KUNUFAIKA NA MIKOPO
Mkurugenzi
Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi
wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waandishi wa
habari(hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya utoaji mikopo kwa mwaka wa
masomo 2014/2015, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi.
Zamaradi Kawawa.
Baadhi
ya Waaandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu
na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw.
Cosmas Mwaisobwa wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Serikali
imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na masomo ya
stashahada maalum ya ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Elimu na Mawasiliano toka
Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati
wa Mkutano na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam.
“
Wanafunzi wapatao 5,000 wanatarajiwa kujiunga na stashahada maalum
katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo wote watanufaika na mikopo ya
elimu ya Juu.”Alisema Mwaisobwa
Akifafanunua, Mwaisobwa alisema kuwa lengo la mpango huo ni kusaidia kuondoa tatizo la walimu wa masomo ya sayansi hapa nchini .
Aidha
Mwaisobwa alibainisha kuwa jumla ya maombi 58,037 ya mikopo yalikuwa
yamepokelewa hadi kufikia Julai 2014 ambapo maombi 37,689 ni waombaji wa
kiume na 19,592 ni waombaji wa kike.
Pia
Mwaisobwa alibainisha kuwa majina ya wanafunzi watakaopata mikopo
kulingana na udahili yatatangazwa kwenye tovuti ya Bodi ambayo ni www.heslb.go.tz .na taarifa hiyo itatangazwa katika vyombo vya habari.
Bodi
ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) inakusanya wastani wa
shilingi bilioni 3 kwa mwezi ikiwa ni marejesho ya mikopo iliyokwisha
tolewa.
View detail
Labels:
Wanufaika na mikopo
Wednesday, August 13, 2014
MOTO MKUBWA WAZUKA KTK MSIKITI WA MTAMBANI
Moto mkubwa umetokea ktk msikiti wa Mtambani uliopo endeo la Kinondoni "B" na kuunguza eneo lote la juu la msikiti huo ambako kunasadikiwa kulikua na madarasa kwa ajili ya shule inayomilikiwa na msikiti huo, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ila inasemekana ulianza ktk chumba kimoja walichokua wanalala wanafunzi wa shule hiyo baadhi wa kike na inasemekana huenda ikawa ni mshumaa ndio ulisababisha moto huo lakini hizi ni tetesi kwa baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo na tunangojea taarifa maalumu kutoka kwa kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni kuthibitisha chanzo cha moto huo. Endelea kutufuatili zaidi kupata taarifa yote ya tukio hili
View detail
Labels:
Ajali ya moto
Subscribe to:
Posts (Atom)
Why Shop on Bongo Online?
We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be